Yanga SC watua na boti ya mapema Dar

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

VINARA katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ambao walifunga mwaka kwa ushindi wa kishindo wa 4-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC jioni ya Desemba 31,2021 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, wamerejea nyumbani baada ya kuuanza mwaka mpya vibaya.

Ni baada ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam jana Januari 10,2022 kuwaharibia mipango yao ya kutetea Kombe la Mapinduzi kwa kuwachapa mabao 9-8 katika dimba la Amaan jijini Zanzibar.
Ilikuwa ni moja ya mchezo wenye ushindani mkubwa ambapo Azam FC wao waliweza kupachika penalti tisa kimiani huku Yanga SC ikifunga penalti nane. 

Penalti tano tano za mwanzo zilikamilika kwa kila timu kufunga jambo lililopelekea kuweza kuanza kupigiana penalti mojamoja. 

Aidha, ngoma ilikuwa nzito kwa kipa Erick Johola kuweza kuokoa penalti sawa na Kigonya Mathias wa Azam FC, lakini ni Yassin Mustapha aliweza kukosa penalti na kuifanya Azam kushinda penalti ya mwisho kupitia kwa Mudhathir Yahya.
Watani wao Simba SC ambao nao waliwafurumusha Namungo FC wanatarajia kukutana na Azam FC katika fainali itakayopigwa Januari 13,2022 katika dimba la Amaan jijini Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments