Yusuph Kileo atumia ubobezi wake katika usalama wa mtandao na uchunguzi wa makosa ya kidijitali kuwajengea uelewa watoto waweze kutumia mitandao kwa manufaa, kujiepusha na matendo ya kihalifu

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MTANZANIA ambaye ni Mtaalam na Mbobezi wa Usalama Mtandao na Uchunguzi wa Makosa ya Kidigitali, Yusuph Kileo ameendelea kutumia utaalamu wake kuyajengea uwezo makundi mbalimbali katika jamii ili yaweze kuneemeka kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Miongoni mwa makundi hayo ni pamoja na watoto ambao wamekuwa wakitumia mitandao kwa kiasi kikubwa kwa sasa.
"Mitandao imekuwa na manufaa mengi na inapotumika vibaya inapekekea changamoto za kihalifu mtandao. Watoto wamekuwa wahanga wakubwa wa uhalifu mtandao.Wanapaswa kulindwa dhidi ya utapeli na dhuluma za kimtandao.

"Nimeshiriki, nikiongoza kampeni maalum ya kutoa elimu ya uelewa kwa watoto waweze kutumia mitandao kwa manufaa na kujiepusha na matendo ya kihalifu mtandao,"amesema Kileo.

Tazama hasara za matumizi mabaya ya mitandao;


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news