BREAKING NEWS: Rais Dkt.Mwinyi atengua uteuzi wa viongozi mbalimbali

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Februari 3, 2022 ametengua uteuzi wa viongozi mbalimbali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi.(Picha na Ikulu).

Hayo ni kwa mujiubu wa taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said.

Mosi, kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt. Mwinyi ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Idara ta Utumishi na Uendeshaji katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, ndugu Omar Ali Omar.

Pili, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Tasisi ya Elimu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, ndugu Suleiman Yahaya Ame.

Tatu, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ametengua uteuzi wa Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, ndugu Fatma Iddi Alli.

Nne, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ametengua uteuzi wa Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, ndugu Fatma Iddi Alli.

Tano, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia na Watoto katika Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news