Madiwani Karatu watakiwa kusimamia miradi ya maendeleo

NA SOPHIA FUNDI

MADIWANI katika Halmashauri ya Wilaya ya Karatu mkoani Arusha wametakiwa kusimamia miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na serikali katika kata zao.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya hiyo, Dadi Kolimba wakati akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri.

Kolimba amesema kuwa, Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo miradi ya Elimu,Afya,Maji na Barabara hivyo ni jukumu la viongozi katika ngazi ya vijiji hadi kata kusimamia miradi hiyo iwe ya kudumu.

Akizungumzia suala la elimu, mkuu wa wilaya aliwataka madiwani kuwahamasisha wazazi wenye watoto umri wa shule kuwapeleka watoto wao shule kwani miundombinu iko ya kutosha ambapo alisema hatapenda kusikia wanafunzi waliofaulu kwenda secondary hawajaenda na wa darasa la Kwanza hawajaandikishwa.
Pia mkuu huyo alizungumzia suala la mapato ya halmashauri ambapo alisema kuwa halmashauri iwe na mikakati mizuri ya ukusanyaji wa mapato ikiwemo kuwa na takwimu halisi ya mapato ili kuweza kupata mapato ya kuendesha miradi ya maendeleo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Karia Magaro aliwaomba madiwani kushirikiana na viongozi wa vijiji na kata kupata takwimu ya vyanzo vya mapato ikiwemo maduka yaliyopo katika maeneo yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news