Hospitali ya Taifa Muhimbili yapongezwa utekelezaji miradi ya fedha za UVIKO-19

>Yasaini mikataba 57 na Wazabuni

NA IRENE THOMSON 

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) imepongezwa kwa hatua ilizofikia katika utekelezaji wa miradi ya afya kutokana na fedha za UVIK0-19 ambapo hadi sasa imesaini mikataba 57 na wazabuni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba mbalimbali.Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi akizungumza na Menejimenti ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (hawapo pichani) wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa miradi inayotekelezwa kwa fedha za Uviko-19.

Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi alipotembelea MNH ili kukagua utekelezaji wa miradi ya fedha za UVIKO-19 ambapo kiasi cha fedha shilingi Bilioni 25,540,868,000 zilizopokelewa hospitalini hapo kwa ajili ya miradi ya MNH na kupewa jukumu la kununua vifaa vya Hospitali za Rufaa za Mkoa Amana, Temeke, Mwananyamala na Tumbi.

Akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru amesema kati ya fedha hizo, MNH ilipangiwa shilingi bilioni 11,876,800,000 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba kama MRI, CT-Scan, Angio suite, vifaa vya ICU, ujenzi na ukarabati wa idara ya magonjwa ya dharura na kitengo cha dharura kwa kina mama wajawazito na nyinginezo. Hadi sasa MNH imesaini mikataba 16 na wazabuni yenye thamani ya shilingi bilioni 11,874,740,103.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na fedha za Uviko-19.

Prof. Museru amesema, Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Temeke ilipangiwa shilingi bilioni 4,071,470,000 kwa ajili ununuzi wa CT-Scan, Digital X-Ray, Portbale Utrasound, vifaa vya ICU, radiolojia, vifaa vya idara ya magonjwa ya dharura n.k. Hadi sasa Temeke imesaini mikataba 11 na wazabuni yenye thamani ya shilingi 3,559,365,995.84.

Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Amana ilipangiwa shilingi bilioni 4,065,490,000 kwa ajili ununuzi wa CT-Scan, Digital X-Ray, Portbale Utrasound, vifaa vya ICU, radiolojia, vifaa vya idara ya magonjwa ya dharura na nyinginezo. 

"Hadi sasa Amana imesaini mikataba tisa na wazabuni yenye thamani ya shilingi bilioni 3,586,829,769,"amesema Prof. Museru.
Wajumbe wa Menejimenti ya Hospitali ya Taifa Muhimbili wakimsikiliza Katibu Mkuu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru (kulia) wakielekea kukagua miradi ya maendeleo.

Kwa upande wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mwananyamala, Prof. Museru amesema kuwa, ilipangiwa shilingi bilioni 1,889,490,000 kwa ajili ununuzi wa Digital X-Ray, Portbale Utrasound, vifaa vya ICU, radiolojia, vifaa vya idara ya magonjwa ya dharura na vinginevyo. Hadi sasa Mwananyamala imesaini mikataba 10 na wazabuni yenye thamani ya shilingi bilioni 1,708,103,228.20.

Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Tumbi ilipangiwa shilingi bilioni 3,641,554,000 kwa ajili ununuzi wa CT-Scan, Digital X-Ray, Portbale Utrasound, vifaa vya ICU, radiolojia, vifaa vya idara ya magonjwa ya dharura na nyinginezo. "Hadi sasa Tumbi imesaini mikataba 11 na wazabuni yenye thamani ya shilingi bilioni 3,530,686,314.96,"amesema Prof. Museru.
Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi Muhimbili, Mhandisi Gaudence Aksante (kushoto) akitoa maelezo kwa katibu mkuu kuhusu maendeleo ya mradi mmojawapo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi akikagua maendeleo ya ukarabati wa Wodi ya Wagonjwa Mahututi (ICU).

Kutokana na maelezo hayo, Prof. Makubi ameonesha kuridhika na taarifa ya Prof. Museru na kuongeza hizi ni dalili za moja kwa moja kwamba utekelezaji wa miradi utakamilika ndani ya muda husika ambao ni Aprili mwaka huu.

“Kasi ya utekelezaji wa miradi inaridhisha nina matumaini makubwa kuwa miradi hii itakamilika ndani ya muda tuliojiwekea na hata kama muda utazidi nina imani haitakuwa zaidi ya wiki ya kwanza ya mwezi Mei, hivyo nawapongeza sana kwa hatua hii muhimu,”amesema Prof. Makubi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news