Makamu wa Rais afungua daraja la Magara

NA MARY MARGWE

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Philip Mpango amefungua Daraja la Magara linalounganisha wilaya za Babati na Mbulu mkoani Manyara.
Wakati mvua zikinyesha baadhi ya wanafunzi walikuwa wanashindwa kwenda Shule ya Sekondari Magara, kutokana na kushindwa kupita kwenye mto kwa sababu ya maji mengi.

Dkt.Mpango akizungumza Machi 16, mwaka huu wakati akizindua daraja hilo amesema ni haki ya wananchi kupatiwa huduma baada ya wao kulipa kodi.

Amewaahidi wananchi wa Mkoa wa Manyara, kujengwa kwa barabara za lami zilizoahidiwa kwenye ilani ya uchaguzi wa CCM.
"Tunzeni daraja hili na kuhifadhi mazingira ili mto Magara usihame kama alivyoagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Seleman Jafo," amesema.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANRODS), Rogatus Mativila amesema daraja hilo limejengwa na kampuni ya China Railway Seventh Group (CRSG) kwa gharama ya shilingi bilioni 12.6.

Mativila amesema daraja hilo lina urefu wa mita 84 na sehemu tatu za mita mbili pembeni na meta 36 katikati na nguzo 70 za kusimika ardhini.

Amesema, wamejenga kalavati kubwa, makalavati madogo 11, mifereji mita 800 na kuweka taa 16 za barabarani.
Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, Daniel Sillo ameishukuru Serikali kwa ujenzi wa daraja hilo ambalo linaunganisha wilaya za Babati na Mbulu.

Mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Magara, Amina Omary amesema kukamilika kwa daraja hilo kutawasaidia kupita kipindi cha mvua kubwa zikinyesha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news