NAIBU WAZIRI MASANJA AISHUKURU SERIKALI KWA KUJENGA MIPAKA KATIKA HIFADHI ZA TAIFA

NA HAPPINESS SHAYO-WMU

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) ameishukuru Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa kutenga fedha za kujenga mipaka katika hifadhi za Taifa nchini.
Ameyasema hayo leo wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mpakani mwa Tanzania na Kenya.

Amesema, mipaka hiyo itasaidia kupunguza migogoro kati ya hifadhi za nchi mbili tofauti, itasaidia kudhibiti mapato yatokanayo na utalii na pia itasaidia kudhibiti majangili.
Aidha, ameipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuchukua jukumu hilo kwa vitendo kujenga akitolea mfano mpaka kati ya Tanzania na Kenya uliojengwa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news