Yanga SC ileeeeeeee

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

YANGA SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kuichapa KMC mabao 2-0.

Ni katika mtanange uliopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam siku ya Machi 19,2022. 
Katika mchezo huo uliohudhuriwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, bao la kwanza la Yanga beki wa zamani wa timu hiyo, Andrew Vincent (Dante) alijifunga dakika ya 39 katika harakati za kuokoa mpira uliounganishwa na mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele.

Aidha, bao la pili akafunga beki Mkongo, Djuma Shaaban dakika ya 52, akiwa ametoka kutia krosi iliyosababisha bao la kwanza.

Matokeo hayo yanaiwezeaha Yanga kufikisha alama 48 katika mchezo wa 18 na kuendelea kuongoza ligi kwa alama 11 zaidi ya mabingwa watetezi, Simba ambao pia wana mechi moja mkononi.

Pia KMC baada ya kichapo hicho inabaki na alama zake 22 za mechi 18, nafasi ya saba.

Hata hivyo,mechi hiyo ilikwenda sambamba na sherehe za kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan madarakani.

Pia viongozi wa Yanga walicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Wasanii na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news