OR-TAMISEMI yatoa maagizo kwa maafisa elimu

*Ni kuhusu upatikanaji wa taarifa sahihi za wanafunzi walioacha shule kwa sababu mbalimbali ili waweze kurudi darasani

NA ASILA TWAHA,OR-TAMISEMI

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Mhe. David Silinde amewataka Maafisa Elimu Watu Wazima wa Mikoa na Halmashauri kusimamia upatikanaji wa taarifa sahihi za wanafunzi walioacha shule kwa sababu mbalimbali ili waweze kurudi shuleni.
Ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Mafunzo Elekezi yanayolenga kuboresha utoaji wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi, lengo likiwa ni kujifunza na namna ya kuzitatua changamoto za elimu.

Mhe. Silinde amewataka wasimamizi wa elimu ya watu wazima kufanya kazi kwa weledi ili nafasi iliyotolewa na Serikali kwa wanafunzi walioacha shule kwa sababu mbalimbali waweze kurudi shule kuendelea na masomo.
Amesema, Serikali inatambua kuwa jamii iliyoelimika yenye maarifa, ujuzi na uzalendo ndio msingi wa maendeleo ya ujengaji wa uchumi hasa ujenzi wa uchumi wa viwanda.

“Haya ni sababu ya usimamizi mzuri wa elimu ya Awali, Msingi Sekondari na Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo rasmi,”amesema Silinde

Aidha, kuwepo kwa Mpango wa Uwiano kati ya Elimu na Jamii (MUKEJA) na Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Watoto Walioikosa (MEMKWA) Mhe. Silinde amesema, Serikali inatambua umuhimu wa elimu ya watu wazima na nje ya mfumo rasmi kupitia Sera ya Elimu ya mwaka 2014 tamko namba 3.3.3.
Mheshimiwa Silinde anasema,hatua hiyo inalenga kutoa nafasi kwa waliokosa fursa katika mfumo rasmi ili kujiendeleza na kutatua changamoto za maisha au kuhitimu katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo.

Amefafanua kuwa, Serikali inaendelea kuboresha mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia ili kupata idadi kamili ya walengwa wa elimu ya watu wazima na nje ya mfumo rasmi, "ninawaelekeza fuatilieni upatikanaji sahihi wa takwimu za elimu ya watu wazima na nje ya mfumo rasmi kwa kuendelea kuutumia mfumo wa BEMIS,"amesema.

Kwa upande wa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Gerald Mweli amewataka viongozi hao kuendelea kusimamia na kufuatilia wanafunzi wote walioacha shule kwa sababu mbalimbali amesema mpaka sasa takwimu zinaonesha zaidi ya wanafunzi 909 wamesharudi shule kuendelea na masomo kati ya hao wapo wenye sababu mbalimbali zikiwemo utoro na ujauzito.
“Nitoe wito hii idadi ya kwa wanafunzi waliorudi darasani kazi kubwa nyie ndio mmeifanya na Serikali ya Mhe. Samia Suluhu Hassan inatambua kazi yenu ndio mana imetoa fursa wanafunzi wote walioacha shule warudi darasani tekelezeni majukumu yenu tunajua bado wengine wapo tumieni taratibu za kazi zenu ili kusiwe na sababu ya mtu kukosa elimu kwa kukosa fursa ambayo Mhe. Rais ameitoa,"amesema.

Aidha, Mhe. Silinde amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmshauri zote kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi na kuzisimamia utekelezaji wake.

Naye Martha Ignatus (Afisa Elimu Watu Wazima) ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha mazingira ya watumishi na kuahidi maelekezo yote wanaenda kuyafanyia kazi na kuahidi upatikanaji sahihi wa takwimu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news