Utabiri wa hali ya hewa Tanzania saa 24 zijazo/Weather forecast March 31st,2022 starting 21:00 tonight

*MAWINGU KIASI, MVUA NA NGURUMO ZINATARAJIWA KATIKA MAENEO MACHACHE NCHINI

NA GODFREY NNKO

UTABIRI wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3 usiku leo Machi 31,2022 unawasilishwa na mchambuzi Daniel Masunga kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kwa mujibu wa TMA, Visiwa vya Unguja na Pemba, Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Kilimanjaro, Morogoro, Lindi, Mtwara, Kigoma, Tabora, Katavi, Ruvuma, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Simiyu na Shinyanga inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Aidha, mikoa ya Manyara na Arusha inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Pia mikoa ya Dodoma na Singida inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Wakati huo huo, upepo wa Pwani unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa kwa Pwani yote kutoka Kusini kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kusini Mashariki kwa Pwani ya Kusini.
Kwa upande wa hali ya Bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi madogo huku matarajio kwa siku ya Jumamosi ya Aprili 2,2022 mabadiliko kidogo yanatarajiwa.

TANZANIA WEATHER FORECAST 31/03/2022:PARTLY CLOUD, THUNDERSHOWERS ARE EXPECTED OVER FEW AREAS
Weather forecast for the next 24 hours starting tonight at 9:00 p.m on 31.03.2022 as presented by weather analyst Daniel Masunga from Tanzania Meteorological Authority (TMA).

Post a Comment

0 Comments