Simba SC yaitafuna RS Berkane الدنيا دوارة و ساهلة تدور عليك

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

الدنيا دوارة و ساهلة تدور عليك (Ulimwengu unazunguka na ni rahisi kukuzunguka) ukiwa ni msemo unaotumiwa sana na mashabiki wa soka nchini Morocco pindi wanapopoteza,msemo huu huenda leo ukatumika sana nchini humo kwa ajili ya kupeana faraja, ingawa tayari vijana wa Kitanzania wamesonga mbele.
Ni hivi karibuni wawakilishi pekee wa Afrika Mashariki na Kati klabu ya Simba ilishindwa kutamba ugenini baada ya kuchapwa mabao 2-0 na wenyeji RSB Berkane. 

Pengine matokeo hayo yaliwasononesha sana mashabiki na wadau wa klabu hiyo kubwa barani Afrika, kupitia mchezo wa Kundi D Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika uliopigwa dimba la Stade Municipal de Berkane nchini Morocco.

Lakini, vijana wale wale, waliofungwa huko Morocco kwa kauli moja wameazimia kutenda mambo makubwa baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya RS Berkane mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo Machi 13, 2022.
Aidha, dakika ya 50 ya mchezo, Kibu Denis Prosper alimtengenezea pasi safi Larry Bwalya ambaye alishindwa kutumia nafasi baada ya kupiga shuti jepesi ambalo liliwekwa mikononi na kipa wa timu hiyo ya kigeni.

Kocha Pablo alifanya mabadiliko dakika ya 62 kwa kumtoa Kibu Dennis Prosper na nafasi yake ilichukuliwa na Bernard Morrison ambaye mpira wake wa kwanza kugusa ulikuwa hatari kwa RS Berkane.

Morrison alipiga shuti kali nje ya 18 ambalo liligonga mwamba na kurudi ndani na kuondolewa na mabeki wa timu pinzani.
Dakika ya 72 Jonas Mkude alipiga shuti kali nje ya 18 ambalo lilipanguliwa na kipa na kuzaa kona ambayo ilichongwa na Bernard Morrison, lakini haikuwa na madhara kwa upande wa pili.

Aidha, Simba SC walifanya mabadiliko kwa kuwatoa Bwalya na nafasi yake ilichukuliwa na Mzamiru Yassin na walimtoa Sakho aliingia Peter Banda.

Wakati RS Berkane walifanya mabadiliko wa wachezaji watano alitoka Sofian Moudane nafasi yake ilichukuliwa na Mohammed Aziz, alitoka Ba akaingia Brahim El Bahraoui, pia walimtoa Tuisila Kisinda nafasi yake ilichukuliwa na Mohammed Farehane.

Pia alitoka Hamza El Mossaoui nafasi yake ilichukuliwa na Chadrack Muzungu Lukombe na walimtoa Mouad Fekkak nafasi yake ilichukuliwa Elmehdi Aubilla.

Mabadiliko hayo kidogo yalionesha upinzani kwa Simba kwani RS Berkane waliweza kupata kona mbili lakini hazikuwa na madhara langoni mwa Simba. Kwa ushindi huo, Simba inafikisha alama saba na kupanda kileleni mwa kundi hilo, ikiizidi alama moja RS Berkane.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news