Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Machi 21, 2022

*Sarafu ya Austria ya Schilling (ATS) inanunuliwa kwa shilingi 146.8 na kuuzwa kwa shilingi 148.1
 
NA GODFREY NNKO

LEO dola ya Australia (AUD) inanunuliwa kwa shilingi 1688.99 na kuuzwa kwa shilingi 1679.55 huku Franka ya Ubeligiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi 50.0613 na kuuzwa kwa shilingi 50.5044.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Machi 21, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Aidha, Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 152.7 na kuuzwa kwa shilingi 154.2 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.01 na kuuzwa kwa shilingi 20.2.

Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21 huku dola ya Marekani nchini ikinunuliwa kwa Shilingi 2287.0 na kuuzwa kwa Shilingi 2309.9.

Aidha,kwa mujibu wa BoT, Paundi ya Uingereza inanunuliwa kwa Shilingi 3004.7 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3035.7 na Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2523.302 na kuuzwa kwa shilingi 2549.46.
Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 359.6 huku ikiuzwa kwa shilingi 363.14 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 19.21 na kuuzwa kwa shilingi 19.39.

Wakati huo huo, Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.21 na kuuzwa kwa shilingi 2.28 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.61 na kuuzwa kwa shilingi 0.64.
Kwa mujibu wa Benki Kuu, Dirham (AED) ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) inanunuliwa kwa shilingi 622.7 na kuuzwa kwa shilingi 628.81 huku sarafu ya Austria ya Schilling (ATS) ikununuliwa kwa shilingi 146.8 na kuuzwa kwa shilingi 148.1.

Post a Comment

0 Comments