Wabunge:Rais Samia hakukosea kutuletea RC Kunenge mkoani Pwani

NA ROTARY HAULE

WABUNGE wa Mkoa wa Pwani wamempigia chapuo mkuu wa mkoa huo, Abubakar Kunenge kwa kusema ni nabii aliyeletwa Pwani kwa ajili ya kuleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo.
Aidha,wabunge hao wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan kwa kufanya chaguo sahihi dhidi ya Kunenge.

Wabunge wametoa kauli hizo katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Pwani pamoja na kikao cha Bodi ya Barabara vilivyofanyika kwa wakati tofauti Machi 3, mwaka huu mjini Kibaha.
Mbunge wa Jimbo la Kibiti, Twaha Mpembenwe (CCM) amesema kuwa, toka Kunenge ateuliwe na Rais kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani anaona maendeleo makubwa yanafanyika.

Mpembenwe amesema kuwa, katika kipindi kifupi cha Kunenge kukaa Pwani ameona mabadiliko katika zao la korosho na ufuta na kusema mazao hayo kwa sasa yamepata heshima ikiwa pamoja na kupandishwa bei ya manunuzi.

Amesema, kupandishwa kwa bei hizo kumeleta tija kwa wakulima kiasi ambacho kimeongeza mhamko zaidi wa kulima mazao hayo, lakini pia hata wabunge wamepata neno la kusema kwa wakulima hao.

"Mimi niseme tu,Pwani tumepata Nabii lakini wewe mwenyewe mkuu wa Mkoa hujui,na tunaamini kwa kasi yako Pwani itakuwa juu zaidi kimaendeleo,"amesema Mpembenwe.

"Mimi nampongeza Mkuu huyu wa Mkoa kwa kazi kubwa na nzuri anayofanya Pwani ,naona maendeleo makubwa yanafanyika hasa katika korosho na ufuta na Mkuu huyu amesimamia vizuri utekelezaji wake,"ameongeza Mpembenwe.

Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Michael Mwakamo (CCM) amesema kuwa, RC Kunenge amekuwa mtatuzi mzuri wa migogoro ya ardhi na ameona jinsi ambavyo anashughulikia changamoto za wananchi.
"Tuna kila sababu ya kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutuletea Mkuu wa Mkoa wa aina hii,kwa hakika amekuwa kiongozi mwenye kupambania maendeleo ya wananchi wake,"amesema Mwakamo.

Aidha,Mwakamo amemshukuru Rais Samia kwa kumleta Kunenge Mkoa wa Pwani kwa kuwa ni chaguo sahihi la Mkoa wa Pwani ambapo ameahidi kuendelea kushirikiana nae katika majukumu yote ya kuwahudumia wananchi.

Nae Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Mwarami Mkenge (CCM) amesema, kazi anayofanya Kunenge inaonekana na Mkoa unakwenda vizuri na kusema spidi hiyo iendelee kwa faida ya wananchi wao.

Mkenge ametumia nafasi hiyo pia kumuomba mkuu huyo kuhakikisha anafanya utaratibu wa kusimamia mizigo inayoshushwa Bandari ya Bagamoyo wakati wa usiku ili ilipiwe ushuru.
Katika kikao hicho Mbunge wa Jimbo la Chalinze ambaye pia Naibu Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ambaye ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ,wameshauri Bandari zilizopo Mkoa wa Pwani zirasimishwe.

Wamesema Bandari hizo zikirasimishwa zitasaidia kuongeza watalii, kuongeza mapato na kukaribisha wawekezaji na hivyo kufikia malengo ya Uchumi wa Blue kama ambavyo Serikali imekusudia.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge,akiwa mwenyekiti wa kikao hicho amesema kuwa,dhamira yake kubwa ni kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika sekta zote.

Kunenge amesema, mabadiliko anayokusudia kuyafanya ameelekeza katika Viwanda,Kilimo,Ufugaji,Uvuvi,na hata katika Sekta za huduma ya jamii ikiwemo maji,elimu,afya , barabara na hata huduma nyingine.

Amesema, usimamizi mzuri wa kisekta utasaidia kutekeleza adhma ya Mkoa ya kuwa na uchumi wa blue huku akisema katika utekelezaji wake lazima hufanyike kwa kufuata sheria na bila kuonewa mtu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news