Waziri Ndalichako akagua maendeleo ya ujenzi ofisi ya wizara Dodoma

NA MWANDISHI MAALUM

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ametembelea na kukagua maendeleo ya awamu ya pili ya ujenzi wa ofisi yake unaoendelea katika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akikagua mradi wa ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi yake Mtumba Jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo leo Machi 21, 2022. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Prof. Jamal Katundu. Kulia ni Mtaalam Mwelekezi kutoka Chuo Kikuu Kishiriki Ardhi Bw. Saudeni Anania.

Akiwa katika ukaguzi huo, Waziri Ndalichako amesisitiza kuongeza kasi ya ujenzi kwa Mkandarasi SUMA JKT ili kuendana na ratiba iliyotolewa na Serikali kukamilisha ujenzi huo.

“Ni dhamira ya Serikali kuona majengo ya ofisi yanakamilika kwa wakati ili watumishi waweze kukaa na kufanya kazi kwa pamoja hali ambayo itaongeza ufanisi wa utendaji kazi wao na utoaji wa huduma wa ofisi hiyo, hivyo ni vyema mkandarasi akaongeza jitihada katika kukamilisha ujenzi huu,” alisema Ndalichako.
Mtaalam Mwelekezi kutoka Chuo Kikuu Kishiriki Ardhi Bw. Saudeni Anania (kulia) akielea jambo wakati ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati) alipofanya ziara katika mradi wa ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi yake Mtumba jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo Machi 21, 2022. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Prof. Jamal Katundu.

Wakati huo huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ametaka Mkandarasi huyo kuhakikisha wanatekeleza mpango mkakati iliyojiiweka ili ujenzi wa ofisi hiyo ukamilike kwa wakati.

Kwa Upande wake, Mhandisi Ujenzi kutoka SUMA JKT, Capt. Khalfan Mturi ameahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na mheshimiwa Waziri. Pia alieleza kuwa wamejipanga kuongeza nguvu kazi ili kufanikisha shughuli hiyo ya ujenzi.
Mhandisi Ujenzi kutoka SUMA JKT, Capt. Khalfan Mturi akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati) alipofanya ziara katika mradi wa ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi yake Mtumba Jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo Machi 21, 2022.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiwa ameambatana na katibu Mkuu katika ofisi hiyo pamoja na Wakurungenzi wa Idara, Vitengo na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Ofisi hiyo walipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma Machi 21, 2022. (Picha na OWM-Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu).

Katika ziara hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Prof. Jamal Katundu, Wakurungenzi wa Idara na Vitengo pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Ofisi hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news