BAKWATA:SIKUKUU YA EID EL FITR ITAKUWA JUMATATU AU JUMANNE

NA DIRAMAKINI

BARAZA Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) linawajulisha Waislamu na Wananchi wote kwa ujumla kuwa SIKUKUU YA EID EL FITR itakuwa siku ya Jumatatu tarehe 02/05/2022 au Jumanne tarehe 03/05/2022 kutegemea kuandama kwa mwezi.
Sherehe za Eid El-fitr kitaifa kwa mwaka huu zitafanyika Mkoa wa Dar es Salaam. Swala ya Eid itaswaliwa katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI BAKWATA Makao Makuu Kinondoni kuanzia saa 1.30 asubuhi.Baraza la Eid litafanyika katika Viwanja vya Karimjee kuanzia saa 8.00 mchana.

Kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania,Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dkt. Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally Mbwana anawatakia Waislamu na wananchi wote maandalizi mema ya Sikukuu hiyo.

Post a Comment

0 Comments