Serikali kufanya jambo kabla ya mwaka wa fedha 2021/2022

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema, Serikali ya Awamu ya Sita itatumia kiasi cha shilingi bilioni 49.4 kwa mwezi kuajiri na kuwapandisha madaraja jumla ya Watumishi wa Umma 125,223 kabla ya mwaka wa fedha 2021/2022 kuisha ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
“Tukisimamia ipasavyo rasilimali watu, rasilimali nyingine zote tulizonazo zitaweza kutumika ipasavyo katika kutuletea maendeleo katika sekta mbalimbali hapa nchini,”amesema Mheshimiwa Waziri Mhagama.

Post a Comment

0 Comments