Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Aprili 13, 2022

NA GODFREY NNKO

LEO Yen ya Japan (JPY) inanunuliwa kwa shilingi 18.3 na kuuzwa kwa shilingi 18.5 huku Randi ya Afrika Kusini (ZAR) ikinunuliwa kwa shilingi 157.7 na kuuzwa kwa shilingi 159.2.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Aprili 13, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Shilingi ya Uganda (UGX) inanunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65 huku Franka ya Burundi (BIF) ikinunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21.

Dola ya Marekani (USD) inanunuliwa kwa shilingi 2287.24 na kuuzwa kwa shilingi 2310.11 huku Paundi ya Uingereza (GBP) ikinunuliwa kwa shilingi 2982.8 na kuuzwa kwa shilingi 3013.5.
Aidha,Euro ya Ulaya (EUR) inanunuliwa kwa shilingi 2491.5 na kuuzwa kwa shilingi 2517.3 huku Yuan ya China (CNY) ikinunuliwa kwa shilingi 359.2 na kuuzwa kwa shilingi 362.8.

Kwa mujibu wa BoT, shilingi ya Kenya (KES) inanunuliwa kwa shilingi 19.8 na kuuzwa kwa shilingi 19.9 huku Franka ya Rwanda (RWF) inanunuliwa kwa shilingi 2.21 na kuuzwa kwa shilingi 2.28.

Dirham (AED) ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) inanunuliwa kwa shilingi 622.8 na kuuzwa kwa shilingi 628.8 huku sarafu ya Austria ya Schilling (ATS) inanunuliwa kwa shilingi 146.8 na kuuzwa kwa shilingi 148.1.
Kwa upande wa Dola ya Australia (AUD) inanunuliwa kwa shilingi 1710.2 na kuuzwa kwa shilingi 1727.7 huku Pula ya Botswana (BWP) inanunuliwa kwa shilingi 198.9 na kuuzwa kwa shilingi 201.4.

Kwa mujibu wa Benki Kuu, dola ya Canada (CAD) inanunuliwa kwa shilingi 1816.8 na kuuzwa kwa shilingi 1816.4 huku Franka ya Ubeligiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi 50.06 na kuuzwa kwa shilingi 50.51.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news