Serikali kutumia Bilioni 49.4/- kuajiri na kupandisha madaraja watumishi 125,223

NA VERONICA MWAFISI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema, Serikali ya Awamu ya Sita itatumia kiasi cha shilingi bilioni 49.4 kwa mwezi kuajiri na kuwapandisha madaraja jumla ya Watumishi wa Umma 125,223 kabla ya mwaka wa fedha 2021/2022 kuisha ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma Aprili 12,2022 kuelezea utekelezaji wa ahadi ya Serikali ya kuajiri watumishi wapya, kupandisha vyeo na kubadilisha kada watumishi kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Mhe. Jenista amesema hayo Aprili 12,2022 jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuelezea utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuhusiana na ajira mpya na usimamizi wa stahiki za Watumishi wa Umma.

Mhe. Jenista ameainisha mgawanyo wa fedha hizo zitakazotumika kuwa, shilingi bilioni 26,297,541,175.00 zitatumika kuajiri watumishi wapya 32,604 na shilingi bilioni 23,078,224,169.50 zitatumika kuwapandisha madaraja watumishi 92,619.

Mhe. Jenista amechanganua ajira hizo kwa mujibu wa vipaumbele vya kisekta ambapo Sekta ya Elimu imetengewa nafasi za ajira 12,035, Sekta ya Afya imekasimiwa nafasi za ajira 10,285, Kilimo nafasi 814, Mifugo nafasi 700, Uvuvi nafasi 204, Maji nafasi 261 na Sheria nafasi 513.

Waziri Jenista ameeleza kuwa mchakato wa ajira hizo utasimamiwa na Wizara husika, pamoja na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Ameongeza kuwa, licha ya kuajiri na kuwapandisha madaraja watumishi hao, Serikali pia itatumia jumla ya kiasi cha shilingi milioni 824,441,522.00 kuwabadilisha vyeo/kada watumishi 6,026 waliotengewa Ikama na Bajeti ya Mishahara kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 kuanzia tarehe 01 Mei, 2022.

“Maamuzi haya ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuwapandisha vyeo na kuwabadilisha kada Watumishi wa Umma bila shaka yataongeza ari, motisha na uwajibikaji wa hiari kwa watumishi wa umma katika kutoa huduma bora kwa wananchi,’’ Mhe. Amesisitiza.
Sehemu ya watendaji wa Ofisi ya Rais - UTUMISHI pamoja na Waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati akielezea taarifa ya utekelezaji wa ahadi ya Serikali ya kuajiri watumishi wapya, kupandisha vyeo na kubadilisha kada watumishi kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Mhe. Jenista amechanganua ajira hizo kwa mujibu wa vipaumbele vya kisekta ambapo Sekta ya Elimu imetengewa nafasi za ajira 12,035, Sekta ya Afya imekasimiwa nafasi za ajira 10,285, Kilimo nafasi 814, Mifugo nafasi 700, Uvuvi nafasi 204, Maji nafasi 261 na Sheria nafasi 513.

Waziri Jenista ameeleza kuwa mchakato wa ajira hizo utasimamiwa na Wizara husika, pamoja na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Ameongeza kuwa, licha ya kuajiri na kuwapandisha madaraja watumishi hao, Serikali pia itatumia jumla ya kiasi cha shilingi milioni 824,441,522.00 kuwabadilisha vyeo/kada watumishi 6,026 waliotengewa Ikama na Bajeti ya Mishahara kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 kuanzia tarehe 01 Mei, 2022. 

“Maamuzi haya ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuwapandisha vyeo na kuwabadilisha kada Watumishi wa Umma bila shaka yataongeza ari, motisha na uwajibikaji wa hiari kwa watumishi wa umma katika kutoa huduma bora kwa wananchi,’’ Mhe.amesisitiza.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) kuzungumza na Waandishi wa habari kuelezea utekelezaji wa ahadi ya Serikali ya kuajiri watumishi wapya, kupandisha vyeo na kubadilisha kada watumishi kwa mwaka wa fedha 2021/2022. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Xavier Daudi.

Amesema, ni wakati muafaka kwa Watumishi wa Umma kuenzi juhudi za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan za kuboresha masilahi ya Watumishi wa Umma kwa kufanya kazi kwa bidii, weledi na bila kushurutishwa katika kuwahudumia wananchi.

Akizungumzia suala la kusogeza huduma karibu na wananchi hususan maeneo ya pembezoni, Mhe. Jenista amezielekeza Mamlaka za Ajira kutoa kipaumbele cha ajira kwenye maeneo hayo ili wananchi wanufaike na huduma zinazotolewa na Serikali kupitia taasisi zake.

Katika kuhakikisha haki inatendeka katika fursa hizo za ajira, Mhe. Jenista ameziagiza Mamlaka za Ajira katika Utumishi wa Umma kuhakikisha wanaendesha michakato ya ajira hizi kwa uwazi, weledi, uadilifu pamoja na kutoa fursa sawa kwa waombaji wote kuweza kushiriki katika mchakato huu na hatimaye Serikali iweze kupata watumishi mahiri na wenye sifa stahiki.
Sehemu ya Wakurugenzi wa Idara na Vitengo wa Ofisi ya Rais – UTUMISHI wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuelezea utekelezaji wa ahadi ya Serikali ya kuajiri watumishi wapya, kupandisha vyeo na kubadilisha kada watumishi kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Aidha, Mhe. Jenista amewataka Waajiri wote nchini kuhakikisha watumishi wa umma wapya wote watakaoajiriwa wanapata mafunzo elekezi (Induction Course) kupitia Chuo cha Utumishi wa Umma kabla ya kupangiwa vituo vya kazi kama ilivyoelekezwa na Serikali, kuwapangia majukumu stahiki watumishi hao na kusimamia ipasavyo rasilimaliwatu iliyopo kwenye maeneo yao ya kazi ili kuleta tija kwa maendeleo ya taifa.

“Tukisimamia ipasavyo rasilimaliwatu, rasilimali nyingine zote tulizonazo zitaweza kutumika ipasavyo katika kutuletea maendeleo katika sekta mbalimbali hapa nchini,” Mhe. Jenista ameongeza.

Ajira mpya 32,604 zilizotangazwa leo na Serikali zimetimiza idadi ya ajira mpya 44,096 zilizoidhinishwa na Serikali ya Awamu ya Sita katika mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo awali, Serikali iliajiri watumishi 12,336 wakiwemo watumishi 11,492 wa ajira mpya na watumishi 844 wa ajira mbadala.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news