Tusiupuuze Muungano-DC Mwakisu

NA RESPICE SWETU

MKUU wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Isack Mwakisu amewataka Watanzania kuwabeza wanaoupuuza Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutokana na manufaa ya muungano huo.
Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isack Mwakisu akishiriki katika zoezi la uchangiaji damu lililofanyika kwenye uwanja wa Umoja mjini kasulu. (Picha na Respice Swetu).

Kanali Mwakisu ameyasema hayo wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kiwilaya katika Uwanja wa Umoja mjini Kasulu.

Amesema kuwa, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioanzishwa na waasisi wa Taifa letu hayati Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Aman Karume, una manufaa makubwa na ni mfano wa kuigwa.

"Kuna nchi nyingi duniani zilizojaribu kuungana, lakini zimeshindwa na sisi tumebaki kama mfano,"alisema.

Mwakisu amezitaja nchi za Senegal na Gambia kuwa miongoni mwa nchi zilizojaribu kuungana na zikashindwa na kuwataka Watanzania kuzidi kuuenzi na kuudumisha muungano wetu.

Awali kwenye maadhimisho hayo, Kanali Mwakisu aliwangoza mamia ya wakazi wa Wilaya ya Kasulu kufanya usafi kwenye kituo cha afya cha Kiganamo na kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo.

Post a Comment

0 Comments