Ushirika wa Machinjio ya Vingunguti waingia lawamani

NA HUGHES DUGILO

WANYABIASHARA wa Nyama Machinjio ya Vingunguti wameulalamikia uongozi wao kwa kushindwa kuitisha mkutano na kusoma mapato na matumizi tangu walivyoshika nafasi za uongozi kwa zaidi ya miaka mitano sasa.
Wafanyabiashara wa nyama katika Machinjio ya Vingunguti wakiwa katika shughuli zao za uuzaji wa nyama katika machinjio hayo yaliyopo Ilala,Dar es Salaam. (PICHA NA HUGHES DUGILO).

Wamesema kuwa, katiba yao inawataka kila baada ya miaka mitatu lazima wafanye uchaguzi wa viongozi ikiwa ni sambamba na kuitisha mkutano wa kawaida wa kusoma mapato na matumizi kwa wanachama.

Akizungumzia malalamiko hayo Aprili 21, 2022 kwenye mkutano uliowakutanisha wanahabari kwa niaba ya wezake, January Jonas amesema wamechoshwa na hali hiyo huku wakiziomba mamlaka zinazohusika kuchukua hatua stahiki dhidi ya viongozi hao. Ambao wamekaa madarakani kwa zaidi ya miaka saba sasa pasipokuitisha mkutano wowote.
Wafanyabiashara wa nyama katika machinjio ya Vingunguti wakifuatilia mahojiano ya wenzao (hawamo pichani) waliokuwa wakihojiwa na wanahabari machinjioni hapo.
January Jonas ambaye ni mfanyabiashara katika machinjio ya Vingunguti akitoa malalamiko yake mbele ya waandishi wa habari juu ya uongozi wao wa ushirika kushindwa kuitisha mkutano mkuu na kusoma taarifa ya mapato na matumizi kwa kipindi cha miaka saba mfululizo toka viongozi hao wachaguliwe kuongoza ushirika huo.
Fredrick Daudi mfanyabiashara Vingunguti.

"Ndugu waandishi wa habari sisi kama wanachama kuna kiingilio pindi tuapoingia kwenye ushirika wetu ambapo kila mwanachama anatoa shilingi 60000, lakini viongozi hawajawahi kusoma mapato na matumizi jambo ambalo linakinzana na katiba yetu,"amesema January.

Ameongeza kuwa, licha ya changamoto hiyo ya uchaguzi na taarifa za mapato na matumizi, lakini pia kuna changamoto zingine mbalimbali zikiwemo za ngozi na damu ambapo wao kama wafanyabiashara wanaona hawatendewi haki sokoni.

Akijibu malalamiko hayo Mwenyekiti wa Umoja wa Ushirika wa Wafanyabiashara, Joel Meshack amekiri kuwepo kwa ucheleweshaji wa kufanyika kwa mkutano na kudai kwamba hiyo imetokana na kachelewa kuijenga ofisi yenyewe.

Pia amesema kuwa, kutokana na hapo awali kuwepo kwa changamoto lukuki, kwa sasa wamejipanga vyema na kuwahakikishia wanachama wao kuwa Aprili 27, mwaka huu watafanya mkutano na baadae watatangaza tarehe ya mkutano mkuu.
Fredrick Ndahani ambaye ni mfanyabiashara katika machinjio ya Vingunguti.
Mfanyabiashara ndani ya machinjio ya Vingunguti Shadrack Mabumo akizungumza kuulalamikia uongozi wao kushindwa kuwasomea taarifa ya fedha ya mapato na matumizi kwa kipindi cha miaka saba wakiwa madarakani.
Mwenyekiti wa Umoja wa Ushirika wa Wafanyabiashara, Joel Meshack akizungumza katika Ofisi za Ushirika huo.

Amewataka wafanya biashara kuwa watulivu wakati viongozi wao wanapopanga kukamilisha kwa michakato mbalimbali ambayo wanayo kwa manufaa ya wanachama wao hao ikiwa pamoja na kuitisha mkutano na kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu.

"Niwahakikishie wafanyabiashara kwamba kila kitu kipo sawa na sisi kama viongozi tupo hatua za mwisho kufanya mkutano na mambo mengine. Nakuhusu wao kama viongozi ni binadamu kama kuna mapungufu mengine ni ya kibadamu, lakini kwa ujumla tuna mambo mazuri kwa ajili ya watu wetu,"amesisitiza January.

Post a Comment

0 Comments