Utabiri wa hali ya hewa Tanzania saa 24 zijazo/Weather forecast April 11th,2022 starting 21:00 tonight

*ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikihusisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.

NA GODFREY NNKO

UTABIRI wa Hali ya hewa saa 24 zijazo kuanzia leo saa tatu usiku Aprili 11, 2022 unaletwa na mchambuzi Godfrey Kazinja kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kwa mujibu wa TMA, mikoa ya Lindi, Mtwara, Dar es Salaam, Tanga na Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Visiwa vya Unguja na Pemba inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika baadhi ya maeneo na vipindi vifupi vya jua.

Mikoa ya Morogoro, Kagera, Geita, Kigoma na Ruvuma inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Mikoa ya Kilimanjaro, Rukwa, Songwe, Iringa, Mbeya na Njombe inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Mikoa ya Katavi, Tabora, Dodoma, Singida, Manyara, Arusha, Simiyu, Shinyanga, Mwanza na Mara inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Aidha, upepo wa Pwani unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa kwa Pwani yote kutoka Kusini kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kusini Mashariki kwa Pwani ya Kusini.

Pia hali ya bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi makubwa kiasi huku matarajio kwa siku ya Jumatano tarehe 13/04/2022 ikitarajiwa mvua kuendelea kwa Pwani yote.

TANZANIA WEATHER FORECAST 11/04/2022:HEAVY PRECIPITATION AT TIMES ARE EXPECTED OVER SOME AREAS OF THE ENTIRE COAST OF THE INDIAN OCEAN (MTWARA, LINDI, TANGA, DAR-ES-SALAAM AND PWANI REGIONS (NCLUDING MAFIA ISLES), TOGETHER WITH UNGUJA AND PEMBA ISLES

Weather forecast for the next 24 hours starting 21:00 tonight 11.04.2022, presented by weather analyst Godfrey Kazinja from Tanzania Meteorological Authority (TMA).

Post a Comment

0 Comments