NA EMMANUEL MBATILO
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt.Dorothy Gwajima ameagiza kukamatwa kwa wale wote ambao wamehusika kumuozesha mwanafunzi wa kidato cha pili (15) shule ya Sekondari Chamazi iliyipo Jijini Dar es Salaam.

Waziri Gwajima ametoa tamko hilo Aprili 18,2022 mara baada ya kufanya ziara katika kata ya Chamazi na kutembelea eneo ambalo alipo binti huyo.
Amesema,kitendo cha kumuozesha mwanafunzi ni kosa kisheria hivyo wale wote ambao wamehusika wanatakiwa kuchukuliwa hatua.
"Wale wote waliohusika, wazazi,washenga na mashuhuda walioshiriki kwenye shughuli ya kumuozesha binti huyu wote wamekiuka sheria ya mtoto na sheria ya elimu ambayo inamtaka mtoto apate nafasi ya kuendelea na masomo,"amesema Waziri Gwajima.
Aidha, katika tukio hilo, Waziri alipokea taarifa ya kulawitiwa kwa mtoto mdogo (4) na baba yake mzazi ambaye kwasasa anashikiliwa na vyombo vya dora.
Pamoja na hayo Waziri Gwajima ameitaka jamii kuhakikisha inatoa ushirikiano wa kutosha pindi wanapoona na kusikia matukio ya unyanyasaji wa kijinsia yanatokea katika jamii.

"Migogoro ya kifamilia ilifanya aone yuko tayari kuolewa licha ya kuwa anasema moyoni hakuwa tayari kuolewa ila alitaka kuondokana na ugumu wa maisha na kigogoro hiyo. Niwaombe wWzazi familia zetu ziwe na umoja ili kuboresha ustawi wa maisha ya watoto wa kike," amesema Mabelya.
Pamoja na hayo Mhe.Mabelya amesema kama manispaa walijipanga vizuri kupitia kamati na hatimaye kuzuia ndoa hiyo ambayo ilikuwa ifungwe.

Kwa upande wake Ofisa Ustawi Manispaa ya Temeke, Bi.Lilian Mafole amesema Aprili 14, 2022 mchana walipigiwa simu na msamalia mwema kuwa mwanafunzi huyo anatarajiwa kufunga ndoa na Maulid Athuman Aprili 15, 2022 saa 2:00 usiku.
"Baada ya kupokea taarifa hiyo niliwasiljana na vitengo tofauti, tukafanya uchunguzi ili kufahamu vizuri mazingira ya tukio na tulifnjikiwa, siku ya tukio saa mbili usiku tulifika eneo la tukio tukiwa timu nzima ikiwemo mkuu wa shule na polisi,"amesema Bi.Mafole.
Amesema mwanafunzi huyo alichukuliwa na kupelekwa katika nyumba maalumu sehemu ambako anaweza kupatiwa huduma za ushauri wa kisaikolojia na kuangalia namna ya kumrudisha shule.

0 Comments