Waziri Bashungwa ateta na Balozi wa Marekani nchini Tanzania

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Tanzania,Dkt. Donald J. Wright na ujumbe wake leo Aprili 5, 2022 jijini Dodoma.
Katika mazungumzo hayo wamejadili masuala mbalimbali ya kukuza ushirikiano katika sekta ya elimu, afya na fursa za kubadilishana taaluma ya elimu kwa wanafunzi kwenda na kuja kusoma katika nchi hizo mbili.

Pamoja na mambo mengine, wamejadili vipaumbele vya maendeleo ambavyo nchi ya Marekani inaweza kusaidia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo mara nyingi misaada ya wahisani huangalia vipaumbele vya mtoaji na siyo mhitaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news