Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi:Miaka 100 ya Mwalimu Nyerere, tumuenzi kwa kudumisha umoja na amani

Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 huko Butiama katika Kijiji cha Mwitongo nchini Tanganyika (Tanzania kwa sasa). Leo Aprili 13, 2022 kama angekuwa hai, Hayati Baba wa Taifa angeungana na Watanzania kusherehekea miaka 100 ya kuzaliwa kwake.

Aidha, Watanzania tunasherehekea miaka 100 ya kuzaliwa kwa Hayati Baba wa Taifa, tukiwa tuna mambo mengi ya kujivunia kutokana na mchango maridhawa alioutoa wakati wa uhai wake katika nyanya mbalimbali kwa Taifa la Tanzania.

Miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na kufanikisha Uhuru wa Tanganyika bila kumwaga damu, jambo alilosifiwa kama kiongozi ambaye alikuwa na maono makubwa kwa Taifa letu.

Pia, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere wakati wa uhai wake alitoa hotuba mbalimbali katika mikutano ya ndani na nje ya nchi wakati wa uongozi wake na hata baada ya kustaafu,ambazo zimekuwa na mchango mkubwa katika masuala ya kisiasa, kiuchumi na kidini na hata kuipa heshima ya kipekee Tanzania. Tujifunze kwa uchache;

''Nilikutana na mama mmoja akaniambia alikuwa akifanya kazi Jumuiya ya Afrika Mashariki, na sisi watu wa Uganda tulikuwa tunajuana kwa makabila yetu, watu wa Kenya walikuwa wakijuana kwa makabila yao, huyu Mkikuyu, huyu Mluhya. Lakini sisi Watanzania hatujui makabila ya watu, nikawambia mama ni wakati huo, sasa hivi Watanzania wanataka kujua makabila yao, ya nini, mnataka kutambika? Majirani zetu walikuwa wanaiga kutoka Tanzania, sasa bila haya na sisi tunataka kuulizana makabila?,"alihutubia Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere katika hotuba yake ya mkutano mkuu wa CCM 1995.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news