Ahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kumbaka mtoto wa miaka minne

NA DIRAMAKINI

MAHAKAMA ya Wilaya Nkasi mkoani Rukwa imemhukumu kifungo cha maisha jela, Bw. Peter Malema (21) mkazi wa Kijiji cha Nkundi kilichopo Kata ya Kipande wilayani humo kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka minne.
Mtuhumiwa hilo lilikuwa kosa la pili la ubakaji.

Akitoa hukumu hiyo Mei 26, 2022 Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya, Benedict Nkomola amesema kuwa, Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo shaka yoyote na kumtia hatiani kwa kosa hilo chini ya Kifungu cha Sheria cha 130 (1) na (2)(e) na kifungu cha 131 (3) Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Upande wa mashitaka ukiongozwa na Waendesha Mashitaka, Denis Chagike na Sedrick Mashauri waliieleza mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Machi 23 ,2021 katika Kijiji cha Nkundi ambapo alimbaka mtoto huyo wa miaka minne na kumsababishia maumivu makali.

Sambamba na hilo waendesha mashitaka hao waliiambia mahakama hiyo kuwa, mtuhumiwa huyo hilo ni kosa lake la pili la ubakaji na katika kosa la kwanza aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na aliondolewa baada ya kushinda rufaa.

Hivyo, waliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mtuhumiwa kwa maana amewahi kukutwa na kosa kama hilo ili iwe ni fundisho kwa watu wengine wenye nia ya kutaka kufanya vitendo kama hivyo.

Upande huo wa mashitaka uliwasilisha mashahidi nane ambao pasipo kuacha shaka yoyote mahakama ilimkuta mtuhumiwa na kosa na ikaamua kumtia hatiani kufungwa kifungo cha maisha jela.

Post a Comment

0 Comments