George Mpole aipaisha Geita Gold Ligi Kuu ya NBC

NA DIRAMAKINI

GEORGE Mpole ameiwezesha timu yake Geita Gold kutoka mkoani Geita kuzoa alama tatu zote dhidi ya Mbeya Kwanza.

Ni katika mtanange wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara iuliopigwa katika dimba la Maji Maji mjini Songea Mkoa wa Ruvuma.
Mtanange huo wa leo, Mpole alifunga bao hilo pekee dakika ya 12 hivyo kumfanya kuwa na mabao 13 katika msimu.

Kwa ushindi huo, Geita Gold inafikisha alama 34 na kupanda nafasi ya nne, ikizidiwa alama mbili na Namungo FC baada ya wote kucheza mechi 24.

Aidha,Mbeya Kwanza hali inazidi kuwa mbaya baada ya kichapo cha leo, ikibaki na pointi zake 21 za mechi 24 na sasa inashika mkia kwenye ligi ya timu 16 ambayo imeonekana kuwa na mvuto mkubwa.

Post a Comment

0 Comments