HALMASHAURI ZATAKIWA KUTENGA PESA ZA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WAVIU

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu,  Mhe. Ummy Nderiananga amepongeza Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka asilimia 3.5 mwaka 2020 hadi kufikia asilimia  3.2 kwa mwaka 2021.
Naibu Waziri Ofisi yaWaziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga akimsikiliza, Bi, Halima Ally Mbabe Muelimisha rika alipokuwa akieleza shughuli wanazofanya katika Konga ya Jiji la Tanga.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye bajeti Mpya ya serikali 2022-2023 itakayoanza mwezi wa saba ameongeza fedha eneo kutoka Billioni 1 Mpaka Bilioni 1.8,”
Naibu Waziri Ofisi yaWaziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza na viongozi na watendaji wa Mkoa wa Tanga alipokuwa akipokea taarifa ya Mkoa huo ya Mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga alipokuwa akipokea taarifa ya Mkoa wa Tanga ya Mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi.

Aidha, Naibu Waziri Mhe. Ummy Nderiananga ameshauri Halmashauri za wilaya kuona umuhimu wa kutenga fedha za Mapambano Dhidi ya Virusi vya Ukimwi. Hii itasaidia kuwawezesha katika miradi ya vikundi vya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi (WAVIU) kufanya shughuli zao za maendeleo vizuri.
Naibu Waziri Ofisi yaWaziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga akiwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bw. Kaspar Mmuya alipotembelea shule ya Msingi Majani Mapana na shule ya Sekondari Nguvu Mali kujionea utekelezaji wa mradi wa TIMIZA MALENGO.

"Wananchi msiogobe kujitokeza kupima virusi vya ukimwi, mpime mjitambue afya zenu. Kama Kauli mbiu inavyosema pima VVU, Jitambue ishi,"alisema Naibu Waziri Ummy.
Naibu Waziri Ofisi yaWaziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga akiwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bw. Kaspar Mmuya alipotembelea shule ya Msingi Majani Mapana na shule ya Sekondari Nguvu Mali kujionea utekelezaji wa mradi wa TIMIZA MALENGO.

“Mabinti mnao toa elimu rika, endeeleni kuwaelimisha mabinti wenzetu. Asilimia kubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi yapo kwa vijana na asilimia 80% ya hao vijana ni mabinti lazima tuendele kuelimishana,"alisema  Naibu waziri Ummy

Naye Naibu katibu Mkuu Bwn. Kaspar Mmuya amesema Baraza la Watu Waoishi na Virusi Vya Ukimwi ambao wamejitokeza na kujitangaza na kusema wako tayari kushirikiana na serikali kutoa elimu (NACOPHA) ni baraza muhimu.
Naibu Waziri Ofisi yaWaziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga akimsikiliza Bi. Bahati Mohamedi Katibu wa Konga jiji la Tanga alipotembelea katika ziara yake kujionea shughuli za kiuchumi za WAVIU.(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

“Hili baraza ni rasilimali kubwa sana kufikia malengo yetu, wanaishi kwa mfano na wanamalengo na wanatusaidia hata wale walioachaa dawa kwa sababu mbalimbali wanawatafuta na kuongea nao na kuwarudisha kwenye dawa alisema, Naibu Katibu Mmuya.

"Ninaomba hizi afua mbalimbali za ukimwi zinazofanyika, maelekezo yatoke mradi wowote unahusu mambo ya ukimwi washirikiane na NACOPHA. Hawa wanauwezo wa kufikia walengwa mpaka ndani kijijini na wanatusaidia kufikia malengo ya taifa kwa kutumia muda vizuri na fedha vizuri,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news