RC Mjema azindua chanjo ya Polio mkoani Shinyanga, atoa wito kwa jamii

NA KADAMA MALUNDE

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Sophia Mjema amezindua chanjo ya ugonjwa wa kupooza (polio) kwa watoto chini ya miaka mitano mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akimpa mtoto matone ya Chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kupooza (Polio) wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga. (Picha na Malunde 1 blog).

Mhehimiwa Mjema amesema, takribani watoto 450,000 wenye umri chini ya miaka mitano mkoani Shinyanga wanatarajiwa kufikiwa/kupatiwa chanjo ya Polio kuanzia Mei 18 hadi Mei 21,2022. 

Chanjo hiyo itatolewa nyumba kwa nyumba na kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya watoto likiendeshwa na timu ya wataalamu 855.

“Niwatoe hofu wazazi wa Mkoa huu wa Shinyanga, Chanjo hii ya Polio ni salama kabisa na haina madhara yoyote, hakikisheni watoto wanapewa chanjo hii, zoezi litafanyika nyumba kwa nyumba na kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya watoto,”amesema.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akimpa mtoto matone ya Chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kupooza (Polio) wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga

Polio ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi cha Polio ambacho huenezwa kwa kula chakula na kunywa maji yaliyochafuliwa na kinyesi cha mtu mwenye ugonjwa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akimuwekea mtoto alama ya kuwa amepata Chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kupooza (Polio) wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga.

Ugonjwa wa Polio huathiri zaidi watoto wenye umri chini ya miaka mitano ambapo dalili za ugonjwa huu ni Homa, mafua,maumivu ya mwili,kichwa na shingo au ulemavu wa ghafla wa viungo vya mwili.
Mwakilishi Wizara ya Afya, Aziz Sheshe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga.
Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga.
Afisa Ufuatiliaji wa Magonjwa ya Milipuko - Shirika la Afya Duniani (WHO) Ofisi ya Tanzania Dkt. George Kauki (kulia), Mwakilishi Wizara ya Afya, Aziz Sheshe (katikati) na Mwakilishi wa OR- TAMISEMI, Carle Silas Lyimo (kushoto) wakiwa kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Mkazi wa Shinyanga Venance Mahona akitoa ushuhuda kuhusu umuhimu wa Chanjo ya polio kwa mtoto wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Mkazi wa Shinyanga Lighness Mnuo akitoa ushuhuda kuhusu umuhimu wa Chanjo ya polio kwa mtoto wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Mkazi wa Shinyanga Betisheba George akitoa ushuhuda kuhusu umuhimu wa Chanjo ya polio kwa mtoto wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Wazazi wakiwa kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Mei 18,2022 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akisalimiana na Mwakilishi Wizara ya Afya, Aziz Sheshe (katikati) Afisa Ufuatiliaji wa Magonjwa ya Milipuko - Shirika la Afya Duniani (WHO) Ofisi ya Tanzania Dkt. George Kauki (kulia) na Mwakilishi wa OR- TAMISEMI, Carle Silas Lyimo (kushoto) wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano Mkoa wa Shinyanga.

Ugonjwa wa Polio hushambulia mishipa ya fahamu hatimaye husababisha kupooza kwa misuli hasa ya miguu, mikono au yote kwa pamoja na mwingine misuli ya kifua inayosaidia kupumua na kusababisha kifo. Polio husababisha ulemavu wa kudumu.

"Kumbuka kila tone la chanjo ya Polio litaiweka Tanzania salama dhidi ya ugonjwa wa kupooza...Mpe Mtoto Matone...Okoa Maisha"

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news