TCRA kutoa masafa, namba maalumu bure kwa watafiti

NA MWANDISHI WETU

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inatoa masafa pamoja namba maalum za kutoa huduma bure kwa watafiti wote watanzania wanaofanya tafiti zinazolenga katika kutumia teknolojia ya mawasiliano kuongeza tija katika shughuli mbalimbali nchini.
Wanafunzi wakiwa katika banda la TCRA katika Wiki ya Maadhimisho ya Ubunifu yanayofanyika jijini Dodoma.

Akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya Ubunifu nchini yanayofanyika mkoani Dodoma Afisa Mkuu wa Mawasiliano na Mahusiano wa TCRA, Mabel Masasi amesema, utaratibu huo unalenga katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhamasisha ufanyaji wa tafiti ambazo zinalenga katika kuleta maendeleo nchini.
Afisa Mkuu Mawasiliano na Mahusiano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akimpa maelezo ya shughuli za mamlaka kwa mteja aliyetembelea maonesho ya Wiki ya Maadhimisho ya Ubunifu yanayofanyika jijini Dodoma. 

Akizungmzia jinsi ya kupata masafa na namba kwa ajili ya utafiti Mabel amesema iwapo watafiti wanafanya utafiti kupitia vyuo basi vyuo vyao vinatakiwa kuwasiliana na mamlaka hiyo ili kuweza kukamilisha taratibu za kupata masafa au namba ya kufanyia utafiti bila kulipia.
Afisa Mawasiliano na Mahusiano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Aika Benson akimpa maelezo ya shughuli za mamlaka kwa mteja aliyetembelea maonesho ya Wiki ya Maadhimisho ya Ubunifu yanayofanyika jijini Dodoma.

 Kuhusu watafiti binafsi wanaotaka kufanya utafiti kwa kutumia rasilimali hizo Mabel amesema watafiti binafsi watatakiwa kwenda kujisajili Costech ambapo kupitia wao wataweza kuombewa rasilimali hizo kwa ajili ya utafiti bila kulipia.

Madhimisho ya ubunifu hufanyika kila mwaka ambapo kauli mbinu ya mwaka huu ni Ubunifu kwa maendeleo endelevu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news