Uzinduzi Royal Tour wafana Zanzibar, Rais Dkt.Mwinyi ampa kongole Rais Samia kwa ubunifu

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan kwa kuja na wazo la kutayarisha Filamu ya ‘The Royal Tour’ yenye lengo la kuitangaza Tanzania kiutalii Duniani.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akifuatilia Uzinduzi wa Filamu ya Tanzania Royal Tour.(kulia kwake)Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Mgeni Hassan Juma, uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki Unguja Jijini Zanzibar leo 7-5-2022, iliyozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi.
Wageni waalikwa na Wananchi wa Zanzibar wakifuatilia Filamu ya Tanzania Royal Tour,iliyozinduliwa leo 7-5-2022 Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja jijini Zanzibar.

Alisema, madhumuhi ya kutayarisha filamu hiyo ni kuitangaza Tanzania katika nyanja za Utalii, Uwekezaji pamoja na Utamaduni, huku akibainisha Tanznaia kuwa na utajiri mkubwa wa rasilimali ikiwemo maeneo ya fukwe, mbuga za wanyama, maeneo ya urithi (mji mkongwe) na mengineyo na hivyo kutoa fursa ya kuvutia Wawekezaji.

Aidha, aliwataka watendaji Serikalini na sekta binafsi, wadau wa Utalii pamoja na wananchi kwa ujumla kujipanga na kutoa huduma bora ili kukidhi mahitaji kutokana na wimbi kubwa la watalii linalotarajiwa kuzuru hapa nchini kutokana na utayarishaji wa filamu hiyo.

Nae, Mwenyekti wa Kamati ya Maandalizi ya Filamu hiyo, Dkt.Hassan Abass alisema filamu hiyo imeandaliwa na kusimamiwa na mabingwa katika usimamizi wa filamu Duniani.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kulia kwake) Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Mgeni Hassan Juma na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na wakiwa na Wake wa Viongozi wakifuatilia Filamu ya Tanzania Royal Tour, iliyozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya Uzinduzi wa Filamu ya Tanzania Royal Tour, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhi Tuzo ya Muigizaji wa Filamu ya Tanzania Royal Tour na (kushoto kwa Rais) Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Utamaduni na Filamu Zanzibar (BASFU) Dkt. Omar Abdalla na (kulia kwa Rais)Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania.Dkt.Kiagho Kilonzo.(Picha na Ikulu
Dkt. Mwinyi ametoa shukurani hizo katika uzinduzi wa Filamu hiyo hapa Zanzibar, hafla iliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip iliopo karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.

Mapema, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Sharrif Ali Sharrif alisema utayarishaji wa filamu hiyo ni jambo linalotoa taswira ya kuimarika kwa Muungano wa Tanzania, huku akibainisha jinsi itakavyofanikiwa kuitangaza Tanzania.

Katika hafla hiyo iliohudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Serikali, akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilali, Makamo wa Pili wa Rais Hemed Sleiman Abdalla pamoja na viongozi mbali mbali, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi alikabidhiwa Tuzo ya uigizaji Bora wa Filamu Tanzania.

Post a Comment

0 Comments