Viongozi, wananchi watoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mama mzazi wa Waziri Balozi Dkt.Pindi Chana, Regina Mlowe

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mama mzazi wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt.Pindi Chana marehemu Regina Mlowe Mei 22, 2022 mkoani Iringa.
Baadhi ya waombolezaji wakishiriki ibada ya mazishi ya mama mzazi wa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi. Dkt. Pundi Chana marehemu Bi. Regina Mlowe katika Kanisa la Romani Katoliki Mshindo mkoani Iringa.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga (wa kwanza kulia) anayefuata ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Marry Masanja wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mama mzazi wa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana marehemu Bi. Regina Mlowe aliyezikwa katika makaburi ya Makanyagio Mei 22 , 2022 mkoani Iringa.
Baadhi ya waombolezaji wakishiriki ibada ya mazishi ya mama mzazi wa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi. Dkt. Pundi Chana marehemu Bi. Regina Mlowe katika Kanisa la Romani Katoliki Mshindo mkoani Iringa .
Baadhi ya Viongozi wa dini katika Kanisa la Romani Katoliki Mshindo mkoani Iringa wakifanya ibada ya mazishi ya mama mzazi wa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi. Dkt. Pundi Chana marehemu Bi. Regina Mlowe katika Kanisa hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana (katikati) akiwasili katika Kanisa la Romani Katoliki Mshindo lililopo mkoani Iringa kuhudhuria iabada ya mazishi ya mama yake mzazi marehemu Bi. Regina Mlowe aliyefariki Dunia Mei 19, 2022.
Mbunge wa Jimbo la Isimani Iringa Vijijini Mhe. William Lukuvi akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mama mzazi wa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana marehemu Bi. Regina Mlowe mkoani Iringa.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali wakishiriki ibada ya mazishi ya mama mzazi wa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana marehemu Regina Mlowe iliyofanyika nyumbani kwake mkoani Iringa.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana (wa kwanza kushoto) akishiriki ibada ya mazishi ya mama yake mzazi marehemu Bi. Regina Mlowe na (wa kwanza kulia) ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Marry Masanja iliyofanyika nyumbani kwa marehemu mtaa wa Chana mkoani Iringa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Post a Comment

0 Comments