Kijana aliyejivika cheo cha Mteule wa Rais adakwa Mbeya

NA DIRAMAKINI

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia,BW.WARREN MAX MWINUKA (20) mkazi wa Makondeko Mbeya Mjini kwa tuhuma za kujifanya, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, JUMA ZUBERI HOMERA akitumia akaunti ya mtandao wa kijamii wa Instagram kwa jina la “juma_homera”.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP ULRICH MATEI amesema,mtuhumiwa alikamatwa Juni 7,2022 majira ya saa 08:00 mchana huko maeneo ya Mama John jijini Mbeya.

"Mtuhumiwa alikuwa akitumia akaunti hiyo kuwaadaa watu kwa kujifanya ni Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na kutoa namba ya simu ya kwake ili wananchi waweze kutoa/kupeleka kero au shida mbalimbali kwake. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika atafikishwa mahakamani,"amesema.

Post a Comment

0 Comments