'Tunamshukuru Mheshimiwa Rais Samia,sasa tunaondoka makazi duni, kwenda makazi bora Handeni'

NA DIRAMAKINI

WAKAZI wa Tarafa ya Ngorongoro iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha ambao wameamua kuhama kwa hiyari yao kwenye eneo la hifadhi wamesema, wanamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa upendo mkubwa aliouonesha kwao kwa kuhakikisha nao wanakuwa na makazi ya kudumu eneo la Msomela wilayani Handeni mkoani Tanga.
Wakizungumza huku wakiwa wanaezua nyumba zao wenywe tayari kwa kuhama wakazi kwa hiyari wamesema walikuwa wanaisubiri fursa hiyo kwa muda mrefu lakini Rais Samia ameitekeleza, hivyo wanamshukuru sana kwa uamuzi wake. 

Mkazi wa Kijiji cha Kimba wilayani Ngorongoro Beatrice Soka amesema amefurahi sana kwasababu kwa muda mrefu walitamani mchakato huo ufanyike lakini ulichelewa.

“Kwa hiyo tamko hili lilipoletwa kwa kweli mimi ni miongoni mwa watu tuliojiandikisha kwa hiyari yangu pamoja na familia yangu kwa ajili ya kwenda huko Msomela". 
“Bahati nzuri nimekwenda huko Msomela na nimerudi jana.Nimeshuhudia mwenyewe kwa macho yangu na akili zangu kwa kweli fursa tuliyopewa na Rais Samia ni ya kipekee, ni ajabu, ni fursa ya upendeleo kwa wana Ngorongoro wote. 

“Kuna shule, huduma ya maji , miundombinu yote na kuna mabwawa ya kutosha, nyumba, mzunguko wa nyumba kuna ekari tatu mbali na mashamba yalipo nje ya pale ekari tano na mama Samia ametuwezesha tuliotoka hapa tuweze kwenda kuendelea na kasi kwani tumepoteza muda".
Kwa upande wake, Pasihaya Parakoi Seseka ambaye ni miongoni mwa wakazi wa Tarafa ya Ngorongoro ambaye amuamua kuhama kwa hiyari yake 

Akizungumza baada ya kushuhudia zoezi hilo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongela amesema, zoezi hilo ni la hiyari na waliyoamua kuondoka wamefikia hatua hiyo baada ya kujadilina na familia zao na kuafiki mpango huo bila kulazimishwa.

Post a Comment

0 Comments