Marekani yaonesha dhamira njema kupaisha filamu za Tanzania

NA JOHN MAPEPELE

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe, Mohamed Mchengerwa akiambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi mekutana na Balozi wa Marekani hapa nchini leo Juni 8, 2022 jijini Dar es Salaam na kujadili masuala mbalimbali ya sekta ya michezo na sanaa ikiwa ni pamoja na ujio wa msanii mashuhuri wa uchoraji,Ashley Collins hapa nchini.
Wakizungumza katika kikao hicho ambacho, Mhe. Balozi wa Marekani nchini Tanzania , Dkt. Donald Wright ameambatana na Afisa Uhusiano wa Ubalozi huo, James Rodriguez wamejadili pia ujio wa timu ya wachezaji nguli wanawake ya mchezo wa kikapu wa Ligi ya NBA nchini Marekani hapa nchini ambao watakuja Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wachezaji wanawake wa mchezo huo hapa nchini.

Mhe.Mchengerwa amesema, viongozi hao wamekubaliana kuendeleza malengo ya Royal Tour kwa kushirikiana zaidi kwenye kuendeleza sekta za sanaa na michezo ikiwemo kuendeleza filamu za hapa nchini za “Swahiliwood” ili ziwe katika kiwango cha Kimataifa kama zile za nchini Marekani kwa kupata walaam ambao watasaidia katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuandaa miswada (script).
Amesema, Tanzania imebarikiwa kuwa na maeneo ya kipekee ya kuchezea filamu ambazo zingeweza kuwa bora na kusisitiza kuwa ni azma ya serikali kujenga mazingira wezeshi ikiwa ni pamoja na kuangalia kodi mbalimbali ili kuwavutia wageni kuja kurekodia hapa nchini.

Aidha, amesema eneo jingine ambalo limejadiliwa ni pamoja na kutoa mafunzo maalum katika eneo la haki miliki na hakishiriki kwa kazi mbalimbali za wasanii ikiwa ni pamoja na tuzo za muziki na kwa upande mwingine amesema wamejadili namna ya kushirikisha wataalam kwenye program maalum ya kuibua vipaji vya wasanii na wanamichezo ya mtaa kwa mtaa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news