Mradi wa maji wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi Simiyu washika kasi

NA MWANDISHI WETU-WM

MRADI wa maji wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi Simiyu maandalizi yake yameshika kasi ambapo hivi sasa kazi ya kuhamisha maeneo ya maziko ili kupisha eneo la bomba kuu la maji litakaloanzia ziwa Victoria inaendelea.
Eneo jipya la maziko likiandaliwa ili kuweza kuhifadhi mabaki yatakayopatikana katika zoezi la kuhamisha eneo la maziko, ili kupisha utekelezaji wa mradi wa maji wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi Simiyu.

Kwa mujibu wa mratibu wa mradi huo Mhandisi Mwajuma Waziri wa Wizara ya Maji amesema kazi hiyo ya kutoa nafasi kwa kuhamisha maeneo ya maziko ni shirikishi na inawahusisha ndugu wa familia pamoja na viongozi wa Serikali za Mitaa katika maeneo yanayohusika.

Mhandisi Waziri amesema jumla ya makaburi 78 yanatarajia kuhamishwa, na hadi leo Juni 20 zaidi ya makaburi 22 yamechimbwa na kuhamishwa mabaki kwa kushirikiana na familia husika, na viongozi wa Serikali za Mitaa, na kuyazika katika maeneo mapya yaliyoanishwa na familia husika, nje ya eneo la bomba kuu. 
Mtaalamu wa Afya, pamoja na ndugu wa karibu wa familia katika moja ya kaburi lililofukuliwa na mabaki ya binadamu kupatikana wakijiridhisha kabla ya taratibu nyingine za kifamilia kufanyika, katika eneo la Nyakabindi, Bariadi. Baadhi ya maeneo ya maziko yanahamishwa ili kupisha utekelezaji wa mradi wa maji wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi Simiyu.
Kazi ya kufukua kaburi ili kuhamisha mabaki ikiendelea katika moja ya eneo la maziko wilayani Itilima.

“Kila familia iliyoadhirika na zoezi hili inapewa asante na serikali, na endapo mabaki hayatapatikana kwasababu yoyote, ikiwamo kukosea alama za mahali lilipo kaburi, wakati wa ujenzi mabaki yakipatikana basi familia husika itapewa stahiki kama ilivyopangwa na Serikali,”amesema.

Mhandisi Waziri amewaambia wakazi wa Itilima wakati wa kuhamisha mabaki yaliyopatikana katika moja ya kaburi, na kuongeza zoezi lote linagharamiwa na Serikali.

Ameongeza kila kaburi litakalochimbwa kutakuwa timu ya wataalamu wa afya watakagua mabaki ili kujiridhisha endapo ni mabaki ya binadamu, ili kuweka uwajibikaji kwa jamii na malipo.
Mmoja wa viongozi wa familia aliyechaguliwa kusimamia zoezi la kuhamisha eneo la maziko, Bw.Saguda Mayenga akipokea asante kutoka Serikalini wa ushirikiano wa familia yake baada ya kubainika kwa masalia katika makaburi matatu eneo la Nyakabindi, Bariadi.
Wataalamu wakichukua takwimu muhimu katika moja ya eneo la maziko kya familia mkoani Simiyu, kabla ya zoezi la kuhamisha kaburi halijaannza.

Mradi wa maji wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi Simiyu ni moja ya mradi wa maji utakaoleta mapinduzi makubwa kwa kuwahudumia wananchi, mifugo na kuendeleza masuala ya kilimo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news