Ofisi ya Waziri Mkuu yavipongeza Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Bw.Kaspar Mmuya amevipongeza Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa kutoa maarifa mbadala kwa changamoto zinazoikabili jamii. Hii inatoa hamasa kwa sababu wanaungana na sera za nchi katika kuongeza fursa za kupata ajira.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu,Bw.Kaspar Mmuya akiwa katika banda la Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia wanawake na Makundi Maalumu linalosimamia vyuo vilivyo chini ya wizara hiyo katika maonesho ya Vyuo vya elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yanaofanyika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu,Bw. Kaspar Mmuya akizungumza katika moja ya banda baada ya kutembelea maonesho ya vyuo vya ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yanayofanyika uwanja wa jamhuri Mjini Dodoma.

“Mafunzo ya Elimu ya ufundi na Mafunzo ya ufundi Stadi yanagusa eneo muhimu sana la vijana, vijana wengi wamepata elimu hii kwa mafunzo ya muda mfupi miezi mitatu, miezi sita, miaka mitatu ambayo yanawawezesha kupata ujuzi mbalimbali katika utendaji kazi pamoja na kutoa vyeti,”amesema.

Amesema hayo alipotembelea Maonesho ya Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo Stadi yanayofanyika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma ambayo yamesaidia kutoa maarifa kwa wananchi kujua fursa za ajira zilizopo katika maeneo yao, lakini pia kusaidia wataalamu wetu kuwa na maarifa yanayoendana na soko la ajira linalohitajika katika Nchi yetu.
Mhadhiri wa Chuo cha Afya Mvumi,Bw. John Mpiluka (kulia) akimuelezea Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Bw. Kaspar Mmuya shughuli zinazofanywa na chuo cha afya Mvumi katika banda lao la maonesho ya vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yanaofanyika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Mmuya ametoa rai kwa wanavyuo na wakufunzi kuendelea kuangalia mahitaji ya jamii ili waweze kuandaa mafunzo ya muda mfupi ili kuweza kuwapatia wananchi ujuzi unaotakiwa utakaosaidia kuzalisha ajira nyingi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mitala na Upimaji, Dkt.Annastelllah Sigweyo amesema, baraza inaangalia program zinazoanzisha zainaendana na uhitaji wa jamii baada ya kufanya utafiti wa eneo husika na kwa kuzingatia ushauri wa wadau.
Dkt. Annastellah Sigweyo (katikati) akieleza shughuli zinazofanywa na Baraza la Taifa la Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) katika maonesho ya Vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yanaofanyika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.

"Tunaangalia uwezo wa chuo kinachotaka kutoa program kama kina uwezo wa kutoa ujuzi husika kwa kuangalia uwezo wa walimu kitaaluma katika kutoa ujuzi, ndipo tunapopitisha mtaala kwa ajili ya chuo husika,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news