Rais Samia afanya uteuzi PPRA,Shirika la Mzinga na Baraza la Masoko ya Mitaji na Dhamana Tanzania

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Juni 5, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Bi.Zuhura Yunus.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Samia amemetua, Dkt. Leonada Raphael Mwagike kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA).

Dkt.Mwagike ni Mtaalam wa Ununuzi na Ugavi, Chuo Kikuu cha Mzumbe, Morogoro. Uteuzi wa Dkt.Mwagike kwa mujibu wa taarifa hiyo utaanza Julai 21, 2022 baada ya Mwenyekiti aliyepo Balozi Dkt.Martern Lumbanga kumaliza kipindi chake cha pili Julai 20, 2022.

Pia amemteua Luteni Jenerali mstaafu Samwel Albert Ndomba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mzinga.

Luteni Jenerali mstaafu Ndomba ameteuliwa kwa kipindi cha pili cha miaka mitatu kuanzia Juni 2, 2022.

Mheshimiwa Rais Samia pia amemteua Jaji Mustafa Kambona Ismail kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Masoko ya Mitaji na Dhamana Tanzania. 

Jaji Ismail anachukua nafasi ya Jaji Fredinand Wambali ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Rufani. Uteuzi huo umeanza Juni 2, 2022.

Post a Comment

0 Comments