RAIS SAMIA ANAMUENZI MWALIMU NYERERE KUREJESHA NAFASI YA TANZANIA KIMATAIFA-RC KAFULILA

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Mkoa Simiyu, David Kafulila amesema kuwa ziara za Mhe. Rais duniani mbali ya faida lukuki za kiuchumi ni za kimkakati kurejesha nafasi ya Tanzania kwenye jukwaa la kimataifa.
Mheshimiwa Kafulila amesema hayo Mei 31, 2022 kwenye mkutano wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Comrade Godfrey Chongolo wilayani Maswa kwa ziara ya siku nne mkoani Simiyu.

"Tanzania kihistoria ni Taifa kubwa, sio la kutazama ndani (Inwardlooking) au kujitazama lenyewe. Ni ' Internationalist', limejengwa hivyo tangu zama za Mwalimu Nyerere na itaendelea kuwa hivyo, na nilazima kulinda heshima hiyo kizazi hadi kizazi.

"Wanaosoma na kufuatilia wanajua, Sisi tulikuwa moja ya mataifa machache kabisa Afrika ambayo iwe Ulaya au Amerika haiwezi kufikiria kufanya jambo lolote kwa Afrika bila kushirikishwa. Hii ni heshima Mwalimu Nyerere aliijenga na Rais Samia anaitafuta, anairejesha, hatupaswi kujidogosha,"amesema Kafulila.

Post a Comment

0 Comments