Wizara ya Habari, UNESCO wapiga kambi Bagamoyo kujadili Mpango wa UNSCDF

NA ROTARY HAULE

WIZARA ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa (UNESCO) wameungana kwa pamoja katika kikao kazi cha ushauri kwa ajili ya uimarishaji wa Matokeo ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari hapa nchini.
Kikao hicho cha pamoja kimeanza kufanyika Mei 31,2022 wilayani Bagamoyo mkoani Pwani kwa kuwashirikisha wadau kutoka Wizara ya Habari,Ofisi ya UNESCO Dar es Salaam,Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa,pamoja na wataalam mbalimbali.
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari Maelezo, Patrick Kipangula.

Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa kikao hicho, Mkurugenzi Msaidizi wa Habari Maelezo, Patrick Kipangula amesema kuwa, kikao hicho cha siku tano kinalenga kuimarisha na kuweka vipaumbele katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo Endelevu wa Umoja wa Mataifa (UNSCDF).

Kipangula amesema kuwa, mpango huo ulizinduliwa Mei 17, mwaka huu na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Philip Mpango ambao utatekelezwa kwa muda wa miaka mitano kuanzia 2022 hadi 2027.

Aidha, Kipangula amesema mpango huo unafafanua na kufanikisha ajenda ya Taifa ya Maendeleo na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs)ili kuthibitisha hatua za kipaumbele kwa maendeleo ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Kipangula ameongeza kuwa, kikao kinachofanyika hivi sasa Wilayani Bagamoyo kinatumika kujenga uelewa kwa Serikali,Umoja wa Mataifa na wafadhili na kubadilishana kwa ushirikiano juu ya hatua zilizopangwa ndani ya mfumo wa UNSCDF.
"Lengo kuu la kikao hiki ni kuunganisha vipaumbele na hatua muhimu katika mfumo wa Mpango wa Maendeleo Endelevu na Marekebisho ya Vyombo vya Habari unaoongozwa na Wizara ya Habari , Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ndani ya UNSCDF,"amesema Kipangula.

Kipangula, amesema pamoja na lengo kuu lakini yapo malengo mahususi ikiwemo kuoanisha wahusika wakuu katika vipaumbele vya Serikali na dira ya mchango wa kisekta kwenye mfumo wa Maendeleo ya Ushirikiano Endelevu wa Umoja wa Mataifa (UNSCDF).

Ametaja malengo mengine kuwa, ni kuweka mikakati yenye mwelekeo wa matokeo shirikishi na mipango ya kuimarisha mchango wa Sekta katika maendeleo endelevu na masuala mengine yanayohusiana.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kutoka UNESCO hapa nchini, Nancy Angulo amesema wameandaa programu ya kutekeleza aina ya Serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa katika kuendeleza maeneo yote ya habari.

Angulo,amesema programu hiyo italenga katika maendeleo ya habari,usalama kwa Waandishi wa habari,nafasi ya Waandishi katika kukuza maendeleo ya nchi na masuala ya Wanawake.

Hata hivyo,Angulo ametaja maeneo mengine yatakayoguswa ni pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi (Climate Change), Ukatili wa Wanawake na Watoto,Demokrasia na uchaguzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news