Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Juni 14, 2022

NA GODFREY NNKO

LEO Dirham ya Umoja wa Falme za Kiarabu (AED) inanunuliwa kwa shilingi 623.7 na kuuzwa kwa shilingi 629.7 huku Schilling ya Australia (ATS) ikinunuliwa kwa shilingi 146.9 na kuuzwa kwa shilingi 148.3.
Kwacha ya Malawi (MWK) inanunuliwa kwa shilingi 2.098 na kuuzwa kwa shilingi 2.25 huku Rupia ya Pakistan (PKR) ikinunuliwa kwa shilingi 10.69 na kuuzwa kwa shilingi 11.28.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Juni 14, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Dola ya Singapore (SGD) inanunuliwa kwa shilingi 1649.3 na kuuzwa kwa shilingi 1649.1 huku Krona ya Sweden (SEK) ikinunuliwa kwa shilingi 225.6 na kuuzwa kwa shilingi 227.8.
Randi ya Afrika Kusini (ZAR) ikinunuliwa kwa shilingi 142.7 na kuuzwa kwa shilingi 144.1 huku dola ya Marekani (USD) ikinunuliwa kwa shilingi 2290.4 na kuuzwa kwa shilingi 2313.4.

Dinar ya Algeria (DZD) inanunuliwa kwa shilingi 16.4 na kuuzwa kwa shilingi 16.5 huku Franka ya Ufaransa (FRF) ikinunuliwa kwa shilingi 308.3 na kuuzwa 311.06.

Lira ya Italia (ITL) inanunuliwa kwa shilingi 1.044 na kuuzwa kwa shilingi 1.054 huku Rupia ya India (INR) ikinunuliwa kwa shilingi 29.4 na kuuzwa kwa shilingi 29.6.

Shilingi ya Kenya (KES) inanunuliwa kwa shilingi 19.56 na kuuzwa kwa shilingi 19.72 huku Euro ya Ulaya (EUR) ikinunuliwa kwa shilingi 2394.9 na kuuzwa kwa shilingi 2419.9.
Shilingi ya Uganda (UGX) inanunuliwa kwa shilingi 0.59 na kuuzwa kwa shilingi 0.62 huku Franka ya Ubelgiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi 50.14 na kuuzwa kwa shilingi 50.58.

Aidha,Won ya Korea Kusini (KRW) inanunuliwa kwa shilingi 1.78 na kuuzwa kwa shilingi 1.79 huku Dinar ya Kuwait (KWD) ikinunuliwa kwa shilingi 7468.4 na kuuzwa kwa shilingi 7532.8

Yuan ya China (CNY) inanunuliwa kwa shilingi 344.9 na kuuzwa kwa shilingi 348.3 huku Yen ya Japan (JPY) ikinunuliwa kwa shilingi 17.08 na kuuzwa kwa shilingi 17.24.

Post a Comment

0 Comments