Waziri Mchengerwa afunguka kuhusu tuzo za BET 2022

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa amesema watazitumia tuzo za BET za mwaka 2022 kuona maeneo ya kuboresha zaidi katika usimamizi wa sekta ya sanaa nchini Tanzania. 
Waziri Mchengerwa ameyasema hayo baada ya kushuhudia Tuzo za BET za mwaka huu 2022 mjini Los Angeles, California, usiku wa kuamkia leo.

“Tumeshuhudia tuzo hizi ikiwa pia ni maandalizi ya sisi kuandaa tuzo kubwa kwa upande wa Afrika za MTV, ambapo sehemu ya waandaaji wake ni hawa hawa wa tuzo za BET na kuna maeneo ya kisera na kimageuzi tu tutaendelea nayo baada ya hapo,” alisema Waziri Mchengerwa.
Awali, Waziri Mchengerwa alikutana na Makamu wa Rais wa Paramount Africa inayosimamia vituo vya burudani vya MTV na shindano la tizo za MAMA, Bw. Monde Twala na kukubaliana kukamilisha michakato mbalimbali za kuipa Tanzania nafasi ya kuwa mwenyeji wa tuzo za MAMA kwa mwaka 2023 na kukubaliana pia uwezekano wa kuileta BET Tanzania huko mbele na kushirikiana zaidi katika sekta za sanaa kwa ujumla.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo aliyeambatana na Mhe Waziri katika tuzo hizo, Dkt. Hassan Abbasi amesema tuzo za BET pia zitaisaidia Tanzania kuboresha tuzo zake za ndani na usimamizi wake kwani nazo zinaweza kuwa kubwa kama za BET.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news