Wizara ya Fedha yaja na matokeo chanya kutoka mashirika, taasisi za Serikali

NA GODFREY NNKO

SERIKALI imesema kuwa, hadi Aprili 2022, ufuatiliaji umefanyika na kubaini kuwa mashirika na taasisi zote za Serikali zina miliki jumla ya kampuni tanzu 57.

Aidha, Mfumo wa Taarifa za Fedha wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTRMIS) umeboreshwa ili kuwezesha upatikanaji wa taarifa za kifedha za kampuni tanzu na kurahisisha usimamizi wake.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) ameyasema hayo leo Juni 7, 2022 wakati akiwasilisha bungeni jijini Dodoma, Makadirio ya Mapato na Matumizi ambapo ameliomba Bunge kuiidhinishia wizara yake bajeti ya shilingi trilioni 14.94.

Kati ya fedha hizo shilingi trilioni 13.62 ni matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 1.32 ni matumizi ya maendeleo kwa mafungu yake nane kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo kwa mwaka wa Fedha 2022/2023.

Anasema hatua hiyo inakuja kutokana na mwaka 2021/22, wizara kujiwekea lengo la kufanya ufuatiliaji na tathmini ya uendeshaji wa kampuni tanzu za mashirika na taasisi za umma pamoja na mashirika 120 yaliyobinafsishwa.

"Vilevile,mwongozo wa uanzishaji, uendeshaji na usimamizi wa kampuni tanzu za taasisi na mashirika ya umma umekamilika na kuanza kutumika,"amesema.

Pia,Mheshimiwa Waziri Dkt.Nchemba amesema kuwa, ufuatiliaji na tathmini imefanyika katika mashirika 98 yaliyobinafsishwa, ikijumuisha hoteli 10, kampuni 31, mashamba 15 na viwanda 42.

Amesema, matokeo ya ufuatiliaji huo yamebaini kiwango kidogo cha uzalishaji wa zao la mkonge, baadhi ya mashamba kutoendelezwa na mengine kutelekezwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news