Global Education Link (GEL) yawamegea siri wanafunzi kusoma nje

NA DIRAMAKINI

WANAFUNZI nchini wametakiwa kuwatumia Global Education Link (GEL) ambao ni Wakala wa Vyuo Vikuu vya Nje ya Nchi ili waondokane na changamoto ya kujiunga na vyuo vikuu ndani na nje ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya 17 ya elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia,Meneja wa Tawi wa GEL, Micky Musa amesema, mwaka huu jukumu kubwa GEL ni kuhakikisha wanatatua changamoto za wanafunzi wanaohitaji kujiunga na vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi.

Amesema, wapo wanafunzi waliokata tamaa za kushindwa kujiunga na vyuo vikuu kwa sababu mbalimbali ikiwemo ya uchumi.

"Sisi GEL tupo hapa kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi ambao wameshindwa kupata msaada wa kielimu,sisi tuna vyuo vikuu vingi vya nje ya nchi na walimu waliobobea wenye uzoefu,"amesema Musa.

Ameongeza kuwa, kwa sasa GEL imejiunga na Benki ya Amana kwa lengo la kuwakopesha wazazi mkopo usiokuwa na riba kwa asilimia 50 hadi 70 ili kuweza kumsaidia mwanafunzi kusoma.

Amesema, mkopo huo mzazi atalipa huku mtoto wake akiendelea na masomo.Musa amesema, GEL ni tofauti na vyuo kwani mzazi anasaidiwa kutafuta chuo pamoja na usafiri na sehemu husika anayoenda kusoma.

"Mzazi wa mwanafunzi anapokuja katika chuo chetu sisi kama GEL tunamshauri mwanafunzi kozi inayofaa kuweza kusomea, lakini shughuli zote zinazomuhusu mwanafunzi ikiwa ni pamoja visa,udahili tunalisimamia wenyewe,"amesema Musa.

Aidha, amesema kwa wanafunzi wataofika katika maonesho hayo akiwa na matokea yake ya kidato cha nne au cha sita anapatiwa udahili akiwa hapohapo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news