Kamisaa wa Sensa ateta na wadau mkoani Shinyanga

NA KADAMA MALUNDE

KAMISAA wa Sensa ya Watu na Makazi Tanzania Bara Mhe. Anne Makinda ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekutana na kuzungumza na wadau mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 4,2022 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Shinyanga yenye lengo la kutoa elimu ya Sensa na kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23,2022.
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Tanzania Bara Mhe. Anne Makinda ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na wadau mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 4,2022 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakati akiendelea kutoa elimu ya Sensa na kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23,2022.
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Tanzania Bara Mhe. Anne Makinda ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na wadau mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 4,2022 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakati akiendelea kutoa elimu ya Sensa na kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23,2022.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Joseph Mkude akizungumza wakati Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Tanzania Bara Mhe. Anne Makinda ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokutana na wadau mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 4,2022 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakati akiendelea kutoa elimu ya Sensa na kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23,2022.

Akizungumza na wadau hao Makinda amesema maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi yanaendelea vizuri huku akisisitiza Uzalendo kwa wananchi ili kufanikisha zoezi hili ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sahihi kwa Makarani wa Sensa.
Makinda ameagiza elimu na hamasa ya Sensa ya watu na makazi iendelee kutolewa kila mahali hadi siku ya Sensa Agosti 23,2022 ili kuhakikisha kila mwananchi anapata taarifa na kuelewa kuhusu Sensa kwa maendeleo ya taifa.

"Siku ya sensa wananchi wanatakiwa kutoa taarifa za ukweli. Msiwafiche watu wenye ulemavu,"amesema Makinda.
"Sensa ya watu na makazi itafanyika Tarehe 23 Agosti. Mkuu wa kaya awe na taarifa za watu waliolala usiku wa Agosti 23,2022. Taarifa za watu wenye ulemavu zikusanywe ili kusaidia serikali kupanga mipango kwa watau wenye ulemavu ili wapate huduma wanazotakiwa wapate,"ameongeza.

"Makarani wa Sensa watafika katika kila kaya. Kwa wale wapangaji wako katika nyumba hizo ni kaya, wewe mwenye nyumba siyo kaya. Mpangaji kwenye nyumba yako atahesabiwa kuwa ni kaya. Kila mtu aliyelala ndani ya mipaka ya Tanzania atahesabiwa,"amesema Makinda.
Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS Pastory Ulimali akitoa elimu ya Sensa ya Watu na Makazi wakati Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Tanzania Bara Mhe. Anne Makinda ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokutana na wadau mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 4,2022 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakati akiendelea kutoa elimu ya Sensa na kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23,2022.

Naye Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Pastory Ulimali amesema Dodoso la Sensa litakusanya taarifa za kaya siyo familia huku akibainisha kuwa siyo lazima mkuu wa kaya awe baba au mama, mkuu wa kaya anaweza kutoa maelekezo kwa mtu mwingine katika kaya kwa niaba ya mkuu wa kaya ili kutoa taarifa kwa makarani wa sensa watakaotembelea kaya husika.
Meneja wa Takwimu Mkoa wa Shinyanga Eliud Kamendu akizungumza wakati Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Tanzania Bara Mhe. Anne Makinda ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokutana na wadau mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 4,2022 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

"Sensa hii inawahusu watu wote awe mgeni au mwenyeji, ilimradi huyo mtu amelala ndani ya mipaka ya Tanzania usiku wa Agosti 23,2022, Kila mtu atahesabiwa. Kila mtu ahesabiwe mara moja tu na kila mmoja afanye uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi ili zoezi hili lifanyike kikamilifu. Na kwa mara ya kwanza nchini Tanzania mbali ya kuhesabu watu pia tutahesabu majengo tukitumia vifaa vya kidigitali - Vishikwambi,"amesema Ulimali.
Mwenyekiti wa SHY TOWN VIP, Mussa Ngangala akizungumza wakati Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Tanzania Bara Mhe. Anne Makinda ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokutana na wadau mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 4,2022 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Shinyanga , Richard Msanii akizungumza wakati Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Tanzania Bara, Mhe. Anne Makinda ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokutana na wadau mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 4,2022 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. (Picha na Malunde 1 blog).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news