Katibu Mkuu Dkt.Jingu ahimiza ufanisi ujenzi mji wa Serikali

NA MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu azitaka Wizara zote kuhakikisha zinasimamia ufanisi na weledi katika ujenzi Awamu ya Pili wa majengo ya Ofisi zao katika Mji wa Serikali Mtumba.
Wajumbe wa kiko cha kujadili maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika Mji wa Serikali Mtumba wakifuatilia kikao hicho.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu akizungumza wakati alipokutana na Wakurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara zote kujadili maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.Kikao kimefanyika katika Ukumbi wa Ofisi hiyo Julai 18, 2022.kulia ni Naibu katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Kaspar Mmuya na kushoto ni Katibu wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma Bw. Meshack Bandawe.

Ameyasema hayo mapema alipokutana na Wakurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara zote katika Ukumbi wa mikutano wa ofisi yake Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wizara hizo zinzojengwa Mtumba Jijini Dodoma. 

Dkt. Jingu alisema,kila wizara inajukumu la kuhakikisha majengo yanajengwa kwa viwango vinavyoendana na thamani ya fedha huku akiwataka kuendelea kufanya kazi kwa uzalendo kama ilivyoelekezwa.
Katibu wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali Kuhamia Dodoma Bw. Meshack Bandawe akieleza maendeleo ya ujenzi Majengo ya Wizara Awamu ya Pili ambapo alieleza umefikia wastani wa asilimia 30 hadi 67 wakati wa kikao hicho.
Mhandisi kutoka NHC, Bakari Mwijarubi akizungumza wakati wa kikao hicho.

“Viongozi wetu na wananchi kwa ujumla wana matarajio makubwa kuona mji wa Serikali unakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa hatutarajii kuwa na delays,”alisema Dkt. Jingu. 

Aidha, alizitaka kila Wizara kuendelea kuzingatia ubora katika kulifanikisha zoezi hilo huku wakiwasimamia wakandarasi na kuhakikisha kila vifaa vinavyonunuliwa vinakaguliwa na timu husika kabla ya matumizi. 

Aliwasihii viongozi hao kuongeza rasilimali watu, vifaa na wataalamu ili kuweza kukamilisha ujenzi wa majengo hayo.
Karani wa Mradi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Qs Idd Msangi akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
Afisa Tawala Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Prisca Shewali akiuliza swali wakati wa kikao hicho.

“Kazi ya ujenzi izingatie viwango vilivyopo, katika hili tumeunda timu mbalimbali za kupitia na kukagua viwango ambapo tumewapa kazi BICO ya kufanya Quality assurance kuona mihimili ya majengo na mifumo mbalimbli ikiwemo ya maji, umeme na TEHAMA inakidhi vigezo hivyo naomba tuwape ushirikiano ili watimize kazi zao,”alisisitiza. 

Hata hivyo, Dkt. Jingu aliwasisitiza kuendelea kutoa taarifa za maendeleo ya ujenzi huo kila ifikapo tarehe 30 ya mwisho wa mwezi na kuwasilishwa katika Ofisi ya Waziri Mkuu ili kujua na kuwa na uhakikika wa kazi inavyoendelea.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kujadili maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika Mji wa Serikali Mtumba wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu (hayupo pichani)
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Matumizi Bora ya Ardhi Wizara ya Kilimo Mhandishi Juma Mdeke akichangia jambo wakati wa kikao hicho.

Katika hatua nyingine aliwasihi kuendelea kutunza miti iliyopandwa katika maeneo ya ofisi zao kwa kuzingati umuhimu wake wa kuboresha mazingira na kuupamba mji huo. 

“Kila wizara ihakikishe inatunza miti iliyopandwa na kuzingatia mikataba ya upandaji wa miti katika Mji wa Serikali,”alisisitiza Dkt.Jingu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news