Kituo cha Afya Mtoa kuneemesha wananchi

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi katika Kituo cha Afya Mtoa kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida mara baada ya kufanya ziara yake ya kikazi wilayani humo.
Taarifa ya kituo hicho inasema kuwa, ujenzi wake mpaka kukamilika utagharimu jumla ya shilingi milioni 662 ambapo unatarajiwa kutatua kero ya wananchi wakiwemo akina mama na watoto kupata huduma umbali unaozidi kilimita 15 kutoka eneo linapojengwa kituo hicho cha afya.

Miundombinu inayojengwa katika kituo hicho ni pamoja na jengo la Mama na Mtoto, Maabara, jengo la upasuaji, chumba cha kuhifadhia maiti, nyumba ya mtumishi na jengo la kufulia.

Post a Comment

0 Comments