Mtoto Ruby Bridges, shujaa aliyeshinda ubaguzi wa rangi shuleni Marekani

NA CHARLES REGASIAN

AKIWA na miaka sita,Ruby Bridges alikuja kuwa maarufu na kuja kuwa mtoto Mmarekani mweusi wa kwanza kumaliza ubaguzi wa rangi wa shule ya wazungu ya Elementary.
Ruby Bridges akisindikizwa na maafisa wa Serikali ya Marekani wakati wakiondoka William Frantz Elementary School, New Orleans, Novemba 1960.(Picha na AP/Shutterstock.com).

Wakati Ruby anaelekea kuanza daraja la kwanza pale shule ya Williams Frantz Elementary huko Orleans Novemba 14, 1960, huku akizungukwa na timu ya maofisa wa serikali,njiani alikutana na kundi matata la wazungu likimpigia kelele na kumtupia vitu mbalimbali yakiwemo mawe.

Mmoja wa wakuu hao, Charles Burks aliyekuwepo kwenye timu ya kumsindikiza Ruby anakumbuka na kueleza ,"ujasiri aliouonesha Ruby kwenye uso wake juu ya chuki iliyooneshwa dhidi yake, kwa mtoto msichana wa miaka sita kwenda kwake shule ngeni, akiwa na wakuu wa serikali wageni pia eneo ambalo hajawahi kufika, alionyesha ujasiri wa hali ya juu sana,hakulia,hakusikitika,alitembea kifua mbele kama askari mtoto vile, wote tulijivunia sana yeye,"alisema Burks. 

Ruby alipoingia pale shuleni aligundua kwamba ilikuwa haina watoto kwa sababu wote waliondolewa tayari na wazazi wao kwa uwepo wake yeye.

Mwalimu pekee aliyemkubali Ruby na kumfundisha alikuwa ni Mwalimu Barbara Henry ambaye alihamia shuleni pale akitokea Boston,Ruby alifundishwa akiwa peke yake kwa mwaka wake wa kwanza shuleni,sababu wazazi wa kizungu waligoma watoto wao kushirikiana darasa moja na mtoto mweusi. 

Mbali na unyanyasaji wa kila siku ambao ulihitaji wakuu wa serikali wale kumsindikiza wakati wa kwenda shule na kurudi kwa muda wa miezi kadhaa, mbali na vitisho kwa familia yake kwa sababu ya kuingilia shule ya wazungu pia baba yake alifukuzwa kazi sababu ikiwa ni hiyo ya kuingilia shule ya weupe.

Ruby alivumilia na kuhudhuria shule, mwaka uliofuata aliporudi kwa ajili ya daraja la pili kundi lile lililokuwa linamsubiri njiani limpopoe kwa vitu na maneno liliondoka, akakuta kuna wamarekani weusi wengine wamejiunga na shule ile.

Hamasa na nguvu ya kuanza kujiunga na shule ile zilikuwa ni mafanikio Kutokana na uvumilivu ,ujasiri wa Ruby ,kuna vitabu vizuri kadhaa kumhusu yeye vikiwemo;
"The story of Ruby Bridges" kwa miaka 4---8. "Ruby Bridges goes to story" kwa miaka 5-----8, nk. Pia kuna filamu kuhusu habari hii ya Ruby inaitwa " Ruby Bridges ".
Ruby Bridges aliyezaliwa Septemba 8, 1954 alikuwa na umri wa miaka sita tu aliposababisha Taifa kumtazama yeye kama mtoto wa kipekee.

Ni katika harakati zake za kupata elimu bora wakati ambapo watu weusi walichukuliwa kama raia wa daraja la pili, Bridges mdogo akawa alama ya haki za kiraia nchini Marekani.

Bridges alipotembelea Ikulu ya Marekani Julai 16, 2011, Rais wa wakati huo Barack Obama alimwambia, "Nisingekuwa hapa leo. Bila michango yako ya mapema katika harakati za haki za kiraia". Bridges amechapisha vitabu kadhaa kuhusu uzoefu wake na anaendelea kuzungumza juu ya usawa wa rangi hadi leo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news