SERIKALI YARIDHISHWA NA UJENZI WA KITUO CHA URATIBU NA UDHIBITI WA MAAFA

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Bw. Kaspar Mmuya ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Uratibu na Udhibiti wa Maafa unaoendelea katika eneo la Ujenzi la Nzuguni B jijini Dodoma unaogharimu zaidi ya shilingi Bilioni mbili.
Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo, Naibu Katibu Mkuu Kaspar Mmuya amesema ofisi yao inasimamia ubora wa shughuli, thamani ya fedha pamoja na kasi ya ujenzi wa miradi hivyo licha ya changamoto ndogondogo zilizopo katika mradi huo ni vizuri mkandarasi akaongeza kasi ya ujenzi wa mradi huo.
“Ni vizuri kutumia kipindi ambacho hakina changamoto nyingi kufanya kazi nyingi kwa uharaka ili changamoto zikija zile ambazo huwezi kuzikabili inakuwa rahisi ambapo umeshafika sehemu ya juu kwa hiyo mimi wito wangu ni kuongeza spidi maana kuongeza spidi ni jambo la kawaida tu ni kuongeza nguvu kazi, kuongeza vifaa na unaongeza muda wa kazi basi,”amesema.
Aidha,Mmuya ameahidi kurudi kutembelea mradi huo ndani ya mwezi mmoja na kumtaka Mkadiriaji wa Majengo Sauden Anania kuhakikisha anampa taarifa ili kushirikiana na ofisi yake na kuifanya kazi kuwa rahisi.

Post a Comment

0 Comments