Serikali yawekeza miundombinu ya kisasa Hospitali ya Micheweni Pemba

Muonekano wa jengo jipya la Hospitali ya Wilaya ya Micheweni Pemba likiendelea na ujenzi wake na ambapo Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameliweka jiwe la msingi la ujenzi wakati wa ziara yake Pemba kutembelea Miradi ya Maendeleo.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi na mkewe mama Mariam Mwinyi wakimskiliza Mjasimriamali wa bidhaa mbalimbali wakati wakitembelea maonesho ya Wajasiriamali wa Mkoa wa Kaskazini Pemba yaliofanyika katika viwanja vya mpira Micheweni Pemba.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo ya Kitaalam ya Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Micheweni Pemba kutoka kwa Mhandisi wa Wizara ya Afya, Ndg. Said Ali Bakari,wakati akitembelea jengo hilo baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wake, kushoto kwa Rais ni mkewe Mama Mariam Mwinyi na kulia kwa Rais ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mhe. Salama Mbarouk na Naibu Waziri Wizara ya Afya Zanzibar, Mhe. Hassan Hafidh Khamis.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Hospitali ya Wilaya ya Micheweni Pemba akiwa na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Hassan Hafidh Khamis na kushoto kwa Rais ni mkewe Mama Mariam Mwinyi.(Picha na Ikulu).

Post a Comment

0 Comments