Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, na mtazamo wa wajenzi huru

NA CHARLES REGASIAN

TUJIFUNZE na kufunua ukweli wa mambo, kwani wengi sisi hatufahamu baadhi ya mambo, alama,herufi, namba, michoro vilivyowekwa sirini kwa karne nyingi sasa, bila kuwa na nia ya kukejeli wala kubeza harakati za wenzetu zenye malengo ya kujenga mustakabali wa Dunia yetu kwa ujumla.
Gideon M. alishawahi kusema kwamba, kazi ni kufunua ukweli wakati wowote, na mahali popote bila kuleta shida yoyote, Siku ya Wanawake Duniani ni muhimu, karne za nyuma huko Athens wanawake hawakuhesabika kama ni binadamu, sensa ilipita kwa kuhesabia wanaume tu (men not women). 

Kwa sasa mambo ni mazuri, kwani wote tupo sawa bali kwa leo tuangalie wapi hii siku ilipotokea, na ilianzishwa kwa malengo gani? Mbali na ustawi wa kumuona mwanamke anaishi Dunia hii na yeye akifurahia maisha ya furaha kama wanaume, juhudi ambazo hata wanaume wapo bega kwa bega kuzitekeleza, yaani 50% kwa 50%.

Harakati za kupigania haki za wanawake duniani asili yake ni wapagani, Kuhani Kadinali Newman wa Kanisa Katoliki, anasema, " The temple,incense,oil lamps, votive offerings, holy water, Holidays, seasons of devotion, processions, blessings of the fields,sacerdotal vestments, images, and statutes...are all of PAGAN ORIGIN "( Pitia The development of the Christian religion cardinal Newman p.359.). 

Hapo akimaanisha, "Hekalu, uvumba ,taa za mafuta, sadaka za nadhiri, maji matakatifu, Sikukuu, vipindi vya kujitoa, maandamano, misafara, kubariki mashamba, alama na masanamu...yote hayo asili yake ni upagani".

Basi hii inamaanisha kwamba sikukuu nyingi, kama siyo zote,tulizonazo leo zimetokana na sikukuu au sherehe za kipagani, kwa kuwa Siku ya Wanawake Duniani husherehekewa kisiasa na kidini. 

Sikukuu ya Wanawake ilianza kusherehekewa nchini Marekani tarehe 28/2/1909, ikijulikana kama National Women's Day. 

Wazo la kuanzisha sikukuu hii lilitolewa na mwanamama Theresa Malkiel wa Chama cha Kisosholist cha Marekani. Ingawa inadaiwa kuwa, Bi.Theresa Malkiel alianzisha sikukuu hii kama kumbukumbu ya mgomo wa wanawake wafanyakazi wa kiwanda cha nguo uliofanyika Machi 8, 1857 mjini New York, lakini ukweli ni kwamba sababu siyo hiyo.

Theresa Malkiel aliyeanzisha Sikukuu ya Wanawake Marekani na baadae ikawa Sikukuu ya Wanawake Duniani. Bi Theresa Malkiel ni mwanamke mwenye asili ya Kiyahudi na raia wa Marekani aliyezaliwa mwaka 1874, huko Urusi na kufariki mwaka 1949, alikuwa mfuasi wa chama cha kisoshalisti kilichoanzishwa na Karl Maxi. 

Kumbuka kwamba mwaka 1842, Karl Maxi alianza kuandika propaganda za mapinduzi kwa ajili ya "League of Trust" akitumaini kusababisha machafuko.
Theresa Malkiel alikuwa ni muumini wa dini ya wajenzi huru. Kwa nini Februari 28? Tarehe 28 ni tarehe muhimu sana sio tu kwa wajenzi huru, bali pia kwa watabiri wa kale wa nyota na wa siku hizi, tarehe 28/2 ilikuwa ni siku ya kusherehekea mungu Dagon kwa wapagani wa zamani.

Alama ya samaki hutumika kwa waliozaliwa tarehe 28/2 na kujulikana kuwa ni watu wenye uwezo mkubwa katika maisha. 

Kwa maana nyingine Bi.Theresa Malkiel alianzisha sikukuu ya wanawake kitaifa tarehe 28/2 katika kusherehekea sikukuu ya mungu Dagon. 

Mwaka 1917, wanawake nchini Urusi walipata haki ya kupiga kura na ndipo tarehe 8/3 ikawekwa Siku ya Wanawake nchini Urusi, kwa nini 8/3? Kwa matumizi ya kanuni ya namba na hesabu tunapata 8+3=11 Tarehe hii ya Machi 8, iliendelea kusherehekewa kama Siku ya Wanawake kwenye mataifa ya kisoshalisti na kikomunisti hadi ilipofika mwaka 1975, ndipo taasisi nyingine ya kutekeleza ajenda za wajenzi huru yaani Umoja wa Mataifa (UN) ikaitambua rasmi na kuifanya kuwa Siku ya Wanawake Duniani.

Hivyo kutoka Marekani kwa Bi.Theresa Malkiel, kuelekea Urusi na kisha kusambaa duniani kote. 

Hivi ndivyo Machi 8, ilivyofanywa kuwa Siku ya Wanawake Duniani. Ikisherehekewa kisiasa na kidini pia. Wakati wanawake wengine wanafanya maandamano barabarani kwenye miji mikubwa duniani kote, wanawake wenzao waumini wa dini ya wajenzi huru hufanya maandamano ndani ya nyumba za ibada kwa wajenzi huru (LODGES).

Lakini siyo ndani ya loji pekee bali hata ndani ya makanisa Siku ya Wanawake huadhimishwa. 

Baadhi ya madhehebu, ikiwa ni pamoja na dhehebu la GCSDA, wao husherehekea siku ya Jumamosi ya kwanza au ya pili ya mwezi wa tatu kutegemea Machi 8, kama Machi 8 ni Jumamosi ikimaanisha Jumamosi ya pili,basi siku hiyo huwa ni Siku ya Wanawake ambapo ibada husimamiwa na wanawake na endapo Machi 8 siyo Jumamosi basi Jumamosi ya kwanza huwa Siku ya Wanawake. 

Hata kwenye taasisi nyingi vikiwemo vyombo vya habari kama Redio na Televisheni wanawake huwa wanaendesha vipindi siku hiyo. Nini lengo la Siku ya Wanawake duniani?.

Kisiasa ni kutetea haki za wanawake na kuwafanya kuwa sawa na wanaume katika nyanja zote. Hata hivyo, kwa wajenzi huru lengo la siku hiyo ya wanawake ni kuwapandisha sio tu kwenye kimo cha wanaume bali kuwa sawa na mungu.

Itakumbukwa kwamba kilichopelekea mama yetu Hawa (Eva) kuanguka ni kule kutamani kuwa sawa na Mungu,maana aliambiwa, "maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huu; mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu..." (Rejea Mwanzo 3:5).

Zipo rangi sita, rasmi ambazo hutumika Siku ya Machi 8. Kila rangi imebeba ujumbe maalum,upo ujumbe uliowekwa wazi ( exoteric meaning) na ujumbe uliofichika unaojulikana kwa waanzilishi wa siku hii (esoteric meaning). 

Kwanza, rangi nyeusi kwa nje inamaanisha mshikamano na nguvu, lakini kwa ndani inamaanisha giza linalomwakilisha shetani.

Pili, rangi nyekundu kwa nje humaanisha mvuto na nguvu, lakini kwa ndani humaanisha umwagaji wa damu. 

Tatu, rangi ya zambarau (purple) kwa nje humaanisha ujasiri na utii katika kutekeleza lengo, lakini kwa ndani imeandikwa, " Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo za ndani za rangi ya zambarau, na nyekundu, "( rejea Ufunuo. 17:4) ambapo mwanamke huyu ni mnyama wa namba 666.

Hii inamaanisha kwamba Machi 8 ni siku ya kumpatia mamlaka mnyama wa namba 666. Nne, rangi nyeupe ,kwa nje humaanisha usafi wa mwanamke, lakini kwa ndani humaanisha utukufu kama utukufu wa mungu, kwamba hatimaye wanawake wataupata utukufu wa mungu.

Kwamba hatimaye wanawake wataupata utukufu wa mungu na kuwa miungu (woman Thou art God). Tano,rangi ya kijani kwa nje humaanisha tumaini,lakini kwa ndani humaanisha uhai na kutokufa. Hii ni imani ya wajenzi huru ya kutokufa kama alivyoambiwa mwanamke wa kwanza.

 "Hakika hamtakufa" (Mwanzo 3:4). Hii ni imani ya umizimu. Na sita,rangi ya pinki ambayo kwa nje humaanisha upendo, lakini kwa ndani humaanisha imebeba ujumla halisi wa harakati za wanawake.

Post a Comment

0 Comments